Saturday, October 31, 2009

MGOSI AIUA YANGA, SIMBA POINTI 30...


BAO pekee la Mussa Hassan Mgosi, leo katika dakika ya 26, liliiwezesha Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga, mbele ya mashabiki zaidi ya 60,000 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mgosi alifunga bao hilo baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Yanga na kuunganisha vyema krosi ya Mganda, Emanuel Okwi, ambaye jana alikuwa mwiba mchungu kwa ngome ya Yanga.
Kwa ushindi huo, mbali na kulipa kisasi cha kufungwa 1-0, Oktoba 26, mwaka jana kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi msimu uliopita, Simba pia imezidi kujiimarisha kileleni, ikifikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 10, yaani imeshinda mechi zake zote.
Kocha wa Simba, Patrick Phiri, alijivunia washambuliaji wake wenye kasi kina Okwi, Mrwanda na Mgosi, waliowapa wakati mgumu mabeki wa Yanga.
Yanga jana ilionekana kuathiriwa na mfumo wake iliotumia, kujaza viungo wengi na kucheza na mshambuliaji mmoja tu, wakati wapinzani wao walikuwa wakishambulia kupitia pembezoni mwa uwanja.
Kocha Kosta Papic, ambaye alipowasili nchini alisema kutokana na mfumo wake wa kushambulia timu yoyote anayoiongoza haiwezi kutoka uwanjani bila kufunga bao, jana alishuhudia mwamuzi Orden Mbaga akipuliza kipyenga cha kuhitimisha mchezo huo, Yanga ikiwa haijaziona nyavu za Simba.
Kipigo hicho kwa Yanga kinawafanya sasa wazidiwe pointi 12 na wapinzani wao hao wa jadi kwenye Ligi Kuu, jambo ambalo sasa litawafanya wasubiri miujiza ili kutetea ubingwa wao.
Simba itaumana na Mtibwa Sugar katika mchezo wake wa kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi, wakati Yanga itamaliza na Prisons yenye ari mpya baada ya kupata kocha mpya, Oscar Dan Korosso.
Simba: Juma Kaseja, Salum Kanoni, Juma Jabu, Kelvin Yondani, Joseph Owino, Mohamed Banka, Danny Mrwandea, Hillary Echesa, Mussa Mgosi, Emanuel Okwi/David Naftali na Ramadhan Chombo/Uhuru Suleiman.
Yanga; Obren Curkovic, Nsajigwa Shdrack, Amir Maftah, Mohamed Bakari, Wisdom Ndhlovu, Athumani Iddi, Mrisho Ngassa, Nurdin Bakari, Boniphace Ambani/Jerry Tegete, Abdi Kassim/Mike Barasa na Kiggi Makassy/Moses Odhiambo.


Phiri amzidi hesabu Papic

MOJA kati ya vitu vilivyoiponza Yanga leo kufungwa 1-0 na Simba, ni mfumo wake wa uchezaji, kujaza viungo wengi uwanjani na kucheza na mshambuliaji mmoja tu, Boniphace Ambani, ambaye msimu huu ameonekana kupoteza makali.
Kosta Papic, kocha wa Yanga, alikwenda kulala jana akijutia mfumo wake huo, kwani mwenzake, Phiri kwa kujaza washambuliaji watatu mbele, Mussa Mgosi, Emanuel Okwi na Danny Mrwanda, kulimpa faida ya ushindi na kufanya mashambulizi mengi pia.
Papic alishindwa hata kutumia mwanya wa Simba kumpoteza mshambuliaji wake Danny Mrwanda, aliyepewa kadi nyekundu dakika ya 52, kwa kumtolea maneno machafu mwamuzi Orden Mbaga akiwa tayari ana kadi ya njano, hivyo kutolewa nje kwa nyekundu.
Papic aliingiza kiungo mwingine uwanjani, Moses Odhiambo, akiwaacha kwenye benchi washambuliaji Jerry Tegete na Mike Barasa.
Mambo yalibadilika kidogo wakati Papic alipowaingiza Tegete na Barasa dakika nane za mwishoni, lakini wakati huo tayari Phiri alikuwa amekwishawaelekeza wachezaji wake kucheza kwa kulinda bao hilo.
Hakika Yanga walitafuta kila njia ya kutafuta bao, tangu Mussa Mgosi alipowatungua dakika ya…, lakini kutokana na kukosa washambuliaji mbele, kila mchezaji aliyepata alitaka kuutengeneza.
Si kama Yanga ilizidiwa mchezo na Simba jana, bali maarifa ya uwanjani na hicho ndicho pekee ambacho kitampa jeuri Phiri.


Kaseja ni kiboko ya Yanga

PAMOJA na ukweli kwamba safu ya ulinzi ya Simba ni madhubuti, lakini pia kipa Juma Kaseja ni shujaa wa kweli langoni, baada ya leo kuokoa michomo mingi ya wazi, ambayo mbele ya kipa ‘wasiwasi’, Yanga ingeweza kuvuna zaidi ya mabao matatu.
Kaseja aliwakatisha tamaa kabisa Yanga, kutokana na kucheza kwa umakini wa hali ya juu, akiokoa michomo ya hatari na kuituliza timu yake kila ilipoanza kupoteana.
Kwa kuweza kudaka vyema na kuifanya Simba ishinde 1-0, Kaseja amedumisha rekodi yake ya kusimama kwenye lango la timu hiyo tangu ajiunge nayo mwaka 2002 kwenye mechi zote za Ligi ikicheza na Yanga bila ya kupoteza mchezo.
Yanga waliweza kupata ushindi mbele ya Simba, Kaseja akiwa langoni mara moja tu, Aprili 20, mwaka 2003, katika mchezo wa kirafiki ulioandaliwa na kampun ya Dika Sharp.
Siku hiyo Yanga ilishinda mabao 3-0, wafungaji wakiwa ni Kudra Omary dakika ya 30, Heri Morris dakika ya 32 na Salum Athumani dakika ya 47.
Zaidi ya hapo, Kaseja amedaka tangu mwaka 2002, kabla ya msimu uliopita kuhamia Yanga kwa mkataba wa msimu mmoja, lakini mara zote hizo amekuwa akishangilia ushindi na wachezaji wenzake wa Simba.
Hata alipokuwa Yanga msimu uliopita, Kaseja aliiongoza kulazimisha sare ya 2-2 na Yanga katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu, baada ya awali Obren Curkovic kudaka vyema na kuifanya Yanga ishinde 1-0.
Alipokuwa Yanga msimu uliopita, Simba haikuweza kufua dafu kwa Watoto wa Jangwani, lakini msimu huu amerejea na kuwafanya Wekundu wa Msimbazi wafufue ubabe wao.
Mapema tu kabla ya mechi hiyo, Kaseja alisema, Yanga hawawezi kuifunga Simba yeye akiwa langoni - na hilo limetimia, je, kwa nini asijiite ni kiboko ya Yanga?


Mgosi ajisafisha Msimbazi
SIMBA walikuwa wamekwishapoteza imani na Mussa Hassan Mgosi - kwamba ni mchezaji ambaye hawezi kuifunga Yanga hata akibaki anatazamana na nyavu, lakini kwa bao lake pekee lililoipa timu hiyo ushindi leo, bila shaka amejisafisha mbele ya viongozi, wanachama na wapenzi wa timu hiyo.Katika mchezo wa kwanza baina ya Simba na Yanga, Oktoba 26, mwaka jana, Mgosi alikosa mabao mawili ya wazi, siku ambayo, Yanga iliibuka na ushindi wa 1-0 kwa bao pekee la Ben Mwalala.
Wakati mchezo wa marudiano unawadia Aprili 19, mwaka huu, Mgosi alikuwa ana mwaliko wa kwenda kufanya majaribio katika klabu ya Mahindra United ya India, hivyo Simba kwa kujua kwamba hata akibakia hawezi kuifunga Yanga, uongozi ulimruhusu kwenda India.
Lakini huko mambo hayakumwendea vizuri Mgosi, akarejea Simba na hatimaye mechi ya kwanza ya Ligi Kuu baina ya miamba hiyo, alikuwa uwanjani na alichokifanya aliwadhihirishia yote ya nyuma yalikuwa bahati mbaya.
Hii ni mara ya pili kwa Mgosi kuifunga Yanga tangu ajiunge na Simba mwaka 2005, akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro. Mara ya kwanza ilikuwa ni kwenye Kombe la Tusker Julai 2, mwaka 2005 wakati Simba ilipoibuka na ushindi wa 2-0 kwenye fainali.
Siku hiyo Mgosi alichokifanya ni kushindilia msumari wa moto kwenye jeneza la Yanga kwa kufunga bao la pili dakika ya 72, kufuatia Emmanuel Gabriel kufunga la kwanza dakika ya 60.

Banka: Si nilisema, Yanga wamefulia


KIUNGO Mohamed Banka, leo baada ya mchezo huo, alikumbusha kauli yake aliyoitoa kwamba; Yanga watake wasitake watafungwa Oktoba 31, mwaka huu, kwani hicho ndicho kilitokea.
Akizungumza na DIMBA, Banka alisema kwamba alijua utakuwa mchezo mgumu, lakini kitu ushindi kwa timu yake Simba alikiona mapema mno.
“Nilijua utakuwa mchezo mgumu, lakini kitu ushindi kwetu nilijua lazima kipo, tulipata upinzani mkali uwanjani, lakini mwishowe timu bora ilitoka kifua mbele,” alisema Banka.
Banka, ambaye huu ni msimu wake wa tatu Simba, tangu ajiunge nayo akitokea Yanga, jana aling’ara licha ya kukabiliwa na upinzani mkali wa viungo vijana wadogo kama Athumani Iddi, Kiggi Makassy, Nurdin Bakari na mkongwe Abdi Kassim.
Wakati anaachwa Yanga, moja ya sababu zilikuwa ni kwamba alitaka fedha nyingi za usajili wake, uwezo wake unaelekea kufikia mwisho, lakini alipotua kwa Wekundu wa Msimbazi, amekuwa kama amezaliwa upya.


Arsenal yapeta England

ARSENAL leo iliibuka kidedea kwenye Ligi Kuu ya England, baada ya kuichapa Tottenham Hotspurs mabao 3-0, katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Emirates, London.
Ushindi huo, umeifanya Arsenal itimize pointi 25, baada ya kucheza mechi 11, hivyo kupanda kileleni kwa muda ikiipiku Chelsea, iliyokuwa ikiongoza Ligi hiyo kwa pointi zake 24. Hata hivyo, Chelsea ilikuwa inamenyana na Bolton jana, mchezo ambao ikishinda inabakia kileleni.
Hadi mapumziko Arsenal ilikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Robin Van Persie dakika ya 42 na Cesc Fabregas dakika ya 43.
Arsenal ilipata bao lake la pili dakika ya 60, mfungaji akiwa ni Van Persie tena, ambaye jana alikuwa mwiba mchungu kwa ngome ya Spurs.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Almunia, Sagna, Vermaelen, Gallas, Clichy, Diaby, Fabregas, Song, Arshavin/Eboue, Van Persie/Ramsey na Bendtner/Eduardo.
Tottenham; Gomes, Bassong, Corluka, King, Assou-Ekotto, Bentley, Huddlestone/Bale, Jenas, Palacios, Keane/Pavlyuchenko na Crouchyellow.



Kaizer Chiefs, Orlando hakuna mbabe

JOHANNESBURG, Afrika Kusini
WAPINZANI wa jadi nchini Afrika Kusini, Kaizer Chiefs na Orlando Pirates, leo wametoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya nchi hiyo, uliofanyika kwenye Uwanja Loftus Versfeld, wenye uwezo wa kumeza mashabiki 94,700.
Katika mchezo huo, kila timu iliumiliki mpira kwa asilimia 50, Kaizer ikilenga mashuti nane langoni mwa Pirates, kucheza faulo tisa, kupata kona tatu na kuokoa hatari mbili, huku wachezaji wake wawili wakipewa kadi za njano.
Pirates yenyewe ililenga mashuti matano langoni kwa Kaizer, kucheza faulo saba, kupata kona tatu, kuotea mara moja, kuokoa hatari tano langoni mwao na mchezaji wake mmoja kupewa kadi ya njano.
Kaizer itaijutia nafasi waliyopata dakika ya 90, wakati Siphiwe Tshabalala alipopiga shuti kwa guu lake la kushoto kutoka umbali wa mita 25, lakini likagonga mwamba.
Pirates nayo ilipata nafasi dakika hiyo hiyo, baada ya Langu Sweswe wa Kaizer Chiefs kumchezea rafu Thembinkosi Fanteni, lakini Lucky Lekgwathi alipokwenda kupiga adhabu ndogo, haikuwa na madhara.
Kikosi cha Kaizer kilikuwa Bartman, Tau, Jambo, Rooi, Dladla, Letsholonyane, Nale, Nengomasha, Sweswe, Tshabalala na Motaung Jnr.
Pirates: Josephs, Jele, Lekgwathi, Thwala, Mahamutsa, Gumbi, Jali, Mabalane, Mashego, Mbuyane na Modise.

HIZI NI SALAMU ZANGU KWAKO MH MKUCHIKA...




NIANZE kwa kumpongeza Waziri Habari Utamaduni na Michezo, Mh. George Huruma Mkuchika na watendaji wote wa wizara wafanyao kazi kwa uadilifu, kwani mabadiliko makubwa yenye kuashiria ufanisi yameonekana kwa kipindi chake tangu apewe wizara hiyo.
Kwa mwelekeo huu, bila shaka kama Mkuchika atabakia kwenye wizara hiyo kwa miaka mitano ijayo, yapo matarajio makubwa kwamba; sekta ya sanaa, michezo na utamaduni wetu vitaimarika kwa kiasi kikubwa.
Miongoni mwa mambo ya hivi karibuni aliyowahi kufanya Mkuchika ambayo yaliwafurahisha Watanzania wengi ni tamko lake la kupiga marufuku maonyesho yote ya filamu kwenye hadhara ya watu, majumba yasiyo rasmi, vibanda, kumbi ndogondogo, hoteli na maeneo ya baa bila kufuata masharti ya jumba la sinema- kwa mujibu wa sheria na 4 ya mwaka 1974 inayotumika nchini.
Katika agizo lake alililitoa mjini Dar es salaam, wakati akizindua Bodi ya Ukaguzi wa Filamu nchini ambayo itakuwa na jukumu la kukagua na kusimamia maonyesho na shughuli za filamu nchini, Mkuchika alisema sehemu nyingi zinazotumiwa kuonyesha filamu hazina leseni halali za kuonyeshea filamu na kuongeza kuwa siyo salama kwa mali na afya za watu.
Alisema athari nyingi tayari zimekwishajitokeza katika jamii yetu na filamu nyingi zimechangia kubomoa na kudumisha Utamaduni wa taifa- na hata kuchangia kwa kiasi kikubwa kubomoa misingi ya amani, upendo, uadilifu, heshima, uaminifu na utu ambao ni utambulisho wa Mtanzania jinsi ulivyokuwa umejijenga na kuenea katika jamii yetu.
Kweli tamko hili limeonekana kupokewa vizuri na wahusika wote waliotajwa wameanza kufuata taratibu- kwani wale ambao wameendelea kufanya mambo kinyume wamekuwa wakikutana na mikono ya sheria.
Hata hivyo, kuna jambo moja tu ambalo pengine wakati ule Mkuchika ama alisahau au alikuwa hajapewa taarifa kabisa kuhusu suala hilo- nalo ni hizi kampuni ndogondogo za hapa nyumbani za kutoa huduma za Televisheni za kulipa, maarufu kama Cable Televisheni, nazo sasa zinatishia amani ya utamaduni na maadili ya Mtanzania.
Kana kwamba hiyo haitoshi, kampuni hizi (siyo zote) pia zimekuwa zikihujumu kwa kiasi kikubwa kazi za wasanii wa Tanzania, kutokana na kuthubutu kuonyesha filamu za wasanii wa nje na ndani bila ya kufuata utaratibu.
Ingawa wakati anatoa tamko lake la kupiga marufuku maonyesho yote ya filamu kwenye hadhara ya watu, majumba yasiyo rasmi, vibanda, kumbi ndogondogo, hoteli na maeneo ya baa bila kufuata masharti ya jumba la sinema- kwa mujibu wa sheria na 4 ya mwaka 1974, hakuwataja watu wa Cable Televisheni, lakini ukweli ni kwamba sheria hii inawahusu na wao pia.
Ila kwa sababu hawakutajwa moja kwa moja, basi wamejihisi wako huru kuwaonyesha filamu wateja wao bila ya kuzingatia sheria namba 4 ya mwaka 1974, lakini ukweli unabaki pale pale- kwa sababu wao wanafanya biashara, kutokana na kupokea ada za kila mwezi kutoka kwa wananchi na kuwapa huduma- basi sheria hii inawahusu.
Juzi nilikuwa nazungumza na msanii mmoja anaitwa Check Budi, akaniambia alikwenda Kahama mkoani Shinyanga na Nzega mkoani Tabora kwa shughuli zake binafasi, huko alikutana na mambo ambayo yapo kinyume na tamko la Mkuchika.
Alisema kuna kampuni za Cable TV zinaonyesha filamu za wasanii wa Tanzania, lakini kwa sababu wanajua huo ni vunjaji wa sheria- inapofia wakati wa kuonyesha filamu hizo- hawatoi nembo ya TV yao.
Kwa nini hawatoi? Nilimuuliza Check, ambaye aliniambia hivi; “Wanajua wakitoa watu watarekodi na kwenda kushitaki, kwa hivyo wanafanya wakijua kabisa wanavunja sheria, watu hawa ni hatari sana, wanaweza kuwa wanaonyesha hata picha za ngono na watu watashindwa kuwachukulia hatua, kwa sababu utapeleka mahakamani ushahidi ambao hauonyeshi ni Cable TV gani? si itakuwa kichekesho,”.
Hivyo ndivyo alivyoniambia Check kuhusu watu hao wanaomiliki Cable TV- namna ambavyo wanamcheza shere Waziri Mkuchika kwa kufanya kile ambacho alikataza lakini kwa kutumia ujanja ujanja.
Kwa kuzingatia kwamba sanaa imeajiri vijana wengi wa taifa hili, ambao pengine bila ya hivyo leo baadhi yao wangekuwa waporaji mitaani, au wafanya uhalifu wa namna yoyote- kwanza hiyo pekee ni sababu tosha ya watu hawa kuchukuliwa hatua.
Kwani kufanya hivyo kunasababisha wateja wao wasinunue tena filamu za wasanii wa nyumbani baada ya kuziona bure kwenye Cable TV- na kama msanii atakuwa hapati mauzo mazuri kwenye kazi yake, je sanaa itakuwa na faida tena kwake?
Na akiachana sanaa akafanye gani- kama ambavyo tunafahamu wasanii walio wengi Tanzania (siyo wote) ni wale ambao elimu zao ni ndogo- katika kuhakikisha wanatafuta sehemu za kujiegesha waweze kuendesha maisha yao wamegundua sanaa.
Mbali na sababu hiyo, kikubwa ni kwamba mfanyabiashara ambaye yupo tayari kuvunuja sheria ili biashara yake iende vizuri, huyo ni hatari sana kwa taifa- kwani anaweza kufanya jambo lolote ili avune zaidi.
Kuna hatari kubwa hawa watu wanaweza kweli kuwa wanaonyesha hata sinema za ngono- wakiamini kwa hivyo ndiyo watavutiua wateja wengi kwenye biashara yao. Ni kwa sababu hiyo namtumia salamu hizi Waziri Mkuchika, ajue kwamba kuna watu wanamcheza shere. Alamsiki.

BUSTA RHYMES ANAYEKUJA KUWASHIKA FIESTA 2009 ONE LUV




NILIPOISIKIA kwa mara ya kwanza sauti yake kwenye matangazo ya kituo cha Radio Clouds, akiwaambia Watanzania kwamba atakuwapo kutumbuiza kwenye Fiesta ya 2009, awali nilidhani ni Ja Rure anakuja tena nchini kutumbuiza kwenye tamasha ambalo aliwahi kutumbuiza mwaka 2006.
Lakini nilipotulia na kusikiliza hadi mwisho wa tangazo hilo— jina lililotajwa lilikwenda sambamba na dhana niliyokuwa nayo ama atakuwa Ja Rule au Busta Rhymes. Kweli, Busta Rhymes anakuja Tanzania kufanya onyesho moja, akiletwa na kampuni ya Prime Time Promotion Limited, chini ya udhamini wa Serengeti Beer na Nokia.
Ama kweli Fiesta ya mwaka huu itakuwa tamu kuliko zote zilizowahi kufanyika, kwani unapomzungumzia Busta unamaanisha mwanamuziki wa Hip hop anayekubalika na watu wa rika na jinsia zote, yaani wake kwa waume, vijana na hata watu wazima.
Hiyo inatokana na muziki wake, jinsi anavyoweza kubadilika kulingana na wakati, jambo ambalo limemfanya aendelee kuwa juu siku zote.
Msikie katika wimbo I Know What You Want aliomshirikisha Mariah Carey: “Baby if you give it to me, I'll give it to you, I know what you want, You know I got it….Baby if you give it to me, I'll give it to you, I know what you want…You know I got it…”.
Busta ni mkali na kwa sababu hiyo ana haki ya kuwa kipenzi cha wapenzi wa muziki ulimwenguni kote.
Kwa wakati huu anakuja Tanzania ni muda mfupi tu tangu atoe wimbo wake mpya uitwao Arab Money Remix, ambao ndani yake amewashirikisha wakali wengine P Diddy, Ron Browz, Swizz Beats, T. Pain, Akon na Lil Wayne. Wimbo huu, jamaa wanataja maneno ambayo mengine yapo kwenye Qur’an tukufu kwa mfano kwenye kiitikio cha pili; wanasema;
Bismillahi r-rahmani r-rahim, Al hamdu lillaahi rabill'alamin (Oooohh),
We gettin' arab money (haha), We gettin' arab money…Bismillahi r-rahmani r-rahim, Al hamdu lillaahi rabiil'alamin (Oooohh) We gettin' arab money (haha), We gettin' arab money.
Hili linaweza likasababisha Busta akawa gumzo zaidi katika ujio wake Tanzania, lakini ukweli ni kwamba jamaa ni mkali tangu na tangu.
Jina Busta Rhymes alitungwa na Chuck D wa kundi la Public Enemy, kutokana na kumfananisha na mchezaji wa zamani wa Ligi ya Taifa mpira Marekani (NFL), George ‘Buster’ Rhymes, lakini mwenyewe jina lake halisi Trevor Tahiem Smith, Jr.
Huyo ni mwanamuziki, mtunzi wa nyimbo na mwigizaji maarufu duniani, Mmarekani mwenye asili ya Jamaica, aliyezaliwa Mei 20, mwaka 1972 ambaye Novemba 7, mwaka huu atafanya vitu vyake mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Busta alizaliwa East Flatbush, huko Brooklyn, wazazi wake wanatokea Jamaica, Cherry Green na Trevor Smith.
Busta alianza muziki akiwa ana umri wa miaka 17 baada ya kujiunga na kundi la Hip hop, lililokuwa likijulikana kama Leaders of the New School akiwa sambamba na jamaa zake wa Long Island, Charlie Brown, Dinco D na Cut Monitor Milo. Walianza kurekodi muziki mwaka 1989 na kufanikiwa kutoa albamu yao ya kwanza A Future Without a Past mwaka 1991 kutoka studio za Elektra Records.
Mwaka 1993, walitopa kitu kingine, kilichokwenda kwa jina T.I.M.E. (The Inner Mind's Eye), lakini kundi hilo lilisambaratika kutokana na wenzake kumwonea wivu Busta kwa sababu ya umaarufu mkubwa aliokuwa amejipatia.
Hivyo mwaka 1996 alitoa wimbo wake wa kwanza kama msanii binafsi uliokwenda kwa jina la Woo Hah!! Got You All in Check am,bao ulikuwamo kwenye albamu yake iliyouza nakala zaidi ya Milioni, The Coming.
Albamu yake ya pili When Disaster Strikes, aliitoa mwaka 1997, ambayo ndani yake ilikuwa ni nyimbo kali kama Put Your Hands Where My Eyes Could See na Dangerous.
Mwaka 1998, Busta alitoa kingine; Extinction Level Event (Final World Front), ambacho kilizua gumzo kutokana na kutabiri kwamba mwaka 2000 ni mwisho wa dunia.
Wimbo wake Gimme Some More uliokuwa unafanana wa Bernard Herrmann – ulishika namba tano katika chati za muziki nchini Uingereza Januari mwaka 1999, wakati April mwaka huo, wimbo mwingine What's It Gonna Be?! Aaliomshirikisha Janet Jackson, uliingia kwenye kumi bora ya chati za muziki za Marekani na Uingereza.
Baada ya Busta kusaini mkataba na J Records, lebo iliyoanzishwa na aliyekuwa bosi wa Arista Records, Clive Davis, alitoa albamu kali, akiendelea kuinukuu Biblia kwenye albamu hiyo aliyoipa jina Genesis. Katika albamu hiyo aliwashirikisha wakali wengine kama Mary J. Blige, P. Diddy, Kelis na wengineo.
Genesis ilibebwa zaidi na nyimbo kama ule aliomshirikisha Kelis, uitwao What It Is, wimbo wake aliotanguliza kutoka kwenye albamu hiyo, Break Ya Neck Novemba mwaka 2001 na wimbo wa mwisho kuutoa, Pass The Courvoisier Part 2, ambao aliwashirikisha watu kama Pharrell na P. Diddy. Lakini pamoja na umaarufu na kuwa na nyimbo hizo kali, albamu hiyo haikuweza kiuvunja rekodi ya mauzo ya albamu yake iliyotangulia.
Mwaka 2002, Busta alitoa albamu yake ya sita It Ain't Safe No More, ambayo ilifanya vizuri ile mbaya, ikiongozwa na wimbo mtamu zaidi aliomshirikisha Mariah Carey na kundi la Flipmode Squad, uitwao I Know What You Want.
Nyimbo nyingine kali kutoka kwenye albamu hiyo zilikuwa Make It Clap, aliomshirikisha Spliff Starr ambao baadaye aliutolea Remix akimshirikisha Sean Paul. Baada ya kutoa albamu hiyo, aliachana na J Records na mwaka 2004 alisaini mkataba na kampuni ya Dr. Dre, Aftermath Entertainment.
Alipojiunga na Aftermath Busta Rhymes alitoa albamu ya saba, The Big Bang, ambayo ilikuwa albamu yake ya kwanza kuuza nakala zaidi ya milioni maishani mwake. Zaidi ya nakala za CD 209,000 ziliuzwa katika wiki ya kwanza tu tangu kutoka kwa albamu hiyo na kuingia kwenye chati za nyimbo 200 za Billboard. Albamu hiyo pia iliibuka kuwa maarufu zaidi ya albamu zake zote nchini Uingereza, ikishika nafasi ya 19.
Nyimbo kali zaidi zilizokuwamo kwenye albamu hiyo ni pamoja na Touch It, I Love My Chick, aliowashirikisha Kelis na Will.I.Am, New York Shit na In The Ghetto. Albamu hiyo ilimpa ulaji wa kushiriki ziara za wakali kama Mariah Carey iliyoitwa The Adventures of Mimi Tour. Busta baada ya hapo aliimba na Eminem wimbo Touch It Remix Part 5 sambamba na kufanya wimbo na Linkin Park, ulioitwa We Made it akiwashirisha pia Jae Millz na Ne-Yo.
Julai 17, 2008, Rhymes aliachana na Aftermath baada ya kutofautiana na Jimmy Lovine na baadaye ikaelezwa atajiunga na Universal Motown, ambayo ilitoa albamu yake ya nane Back on My B.S. Mei 19, mwaka huu sambamba na kushiriki albamu ya kwanza ya Asher Roth, iitwayo Asleep in the Bread Aisle.
Busta Rhymes alitoa albamu yake ya nane Back on My B.S. Mei 19, mwaka huu akiwa na Universal Motown, ambayo ilishika namba tano katika chati za nyimbo 200 za Billboard, ikiuza nakala 56,000 katika wiki ya kwanza na hadi sasa imekwishauza nakala 122,000. Nyimbo ambazo amekwishatoa kutoka kwenye albamu hiyo ni Arab Money aliowashirikisha Ron Browz, Hustler's Anthem '09, aliomshirikisha T-Pain na Respect My Conglomerate. Wimbo World Go Round, aliomshirikisha mwimbaji Muingereza Estelle, aliutoa nchini Ufaransa Aprili 6, mwaka 2009 kabla ya kuutambulisha na Uingereza Julai 13, mwaka huu.
Kutokana na mgogoro wa utumiaji maneno kwenye wimbo Arab Money, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) uliifungia albamu hiyo, Back on My B.S. ambayo ilisambazwa kimataifa.
Kwa mujibu wa Baraza la Habari la Taifa (Marekani), mashairi ya wimbo huo yanawadhalilisha Waarabu na Waislamu, hivyo kunyimwa ruhusa ya kuisambaza albamu hiyo. Baadhi ya ma-DJ, wasanii na mashabiki wameushambulia wimbo huo wakisema unaudhalilisha Uarabu.
Walisema kwamba sehemu ya wimbo huo katika Remix inanukuu Quran tukufu.
Hivi karibuni wakati wimbo huo ulipotolewa, DJ Dany Neville na rapa wa Iraqi, The Narcicyst walikasirishwa na wimbo wa Busta Rhymes ambao waliurekodi kama jibu. Baadaye Busta aliomba radhi kwa usumbufu wowote aliousababisha. Ma-DJ nchini humo walisema kwamba, japokuwa hawajapata taarifa yoyote ya kuupiga marufuku wimbo huo kwenye klabu za usiku, lakini hawawezi kuupiga. “Siuchezi wimbo Arab Money kwa sababu umeonyesha dharau kwa Waarabu. Sidhani kama umefungiwa kuchezwa kwenye klabu, lakini wengi hapa hawaupigi kwa vyovyote,” alisema DJ Saif wa Dubai.
Lakini wakati hayo yakiendelea, Busta alitangaza juu ya ujio wa albamu yake ya tisa itakayojulikana kama The Chemo. Alisema kwa asilimia 80 albamu yake mpya imekwishakamilika, kazi kubwa ikifanywa na mtayarishaji wa Canada, Boi-1da. Yote kwa yote, Busta atakuwapo Dar es Salaam, kuwapa raha Watanzania katika Fiesta ambayo mwaka huu imepewa kaulimbiu ya One Love. Karibu Tanzania Busta.


WIMBO ULIOLETA BALAA NI HUU HAPA;
BUSTA:
Ayo somebody tell steven speilberg & george lucas
Thank you for directing this movie (hahahaha) (hashemeke hayla ha-its the remix!)

KIITIKIO x2
Bismillahi r-rahmani r-rahim, Al hamdu lillaahi rabill'alamin (Oooohh)
We gettin' arab money (haha), We gettin' arab money
Bismillahi r-rahmani r-rahim, Al hamdu lillaahi rabiil'alamin (Oooohh)
We gettin' arab money (haha), We gettin' arab money

BUSTA
you can talk about your money but i really dont care
im into coppin streets shit im trying to buy air
im the first black nigga that i rap trillionaire
i control heat i'm bout to buy the ozone layer
im into coppin minerals now diamonds and granite
so much paper i could probably gift wrap a planet
and clone a million janet's respect my company
asalamalaikumarahmatullahe wa barakatuhu

KIITIKIO x2

P DIDDY
ayo busta we gettin this money for a long time mayne
check this out
allahamdulliah with my billions pilin
im just wildin, bought two islands
lakshmi makalen
diamond soundin
bout to buy japan, trick im just stylin
money insane
my generals poppin bottle
i was buyin out planes just to fly around spain
fuck a recession im still investin
bout to buy dubai and swim in the shark section
get the dark section (its the remix)
bitch thats the barack section

KIITIKIO x2 (we gettin bad boy money)

RON BROWZ
catch me in da coop that cost a hundred thous,
hakala shikmina lady ron browz
my money make noise yours quite as a mouse
send a email in da boyz in da house
all da girls love me, ya pop bubbly.
hakalashikrhi shorty damn ugly
findin me in the dance floor doin the dougie
trucks sittin too next to yo buggy

KIITIKIO
UBETI WA NNE Swizz Beats
dont even call me swizz no more
call me kaseem dean ?
when i come thru hit you with the brand new
buggati coupe, damn thing only only sits 2
but you know who who ridin in my passenger
side with me flyin shit 2.5 in it, hey hey hey
im in my jeezy watchin tv she call me her habibi
while she feedin me linguini
left right left right and arab dance poppin right
swizz beats busta, money money buss pipes

KIITIKIO x2

T PAIN
Nappy Boy (halalalla)
i let my chain hang down with the best of dem
teddy pain rain down on the rest of dem
misses troopa man heavy holly
get em man, about a man, rubber band, droppin money
bombs like a taliban (hallalla) we gettin arab money (money)
u want this hook you gon' pay dat money
save dat money give it to my kids, ill take that hundred
give her all my kids like (hallalallalalalallaaaaaaaaaa swag)

KIITIKIO x2 (swaggg swagg)

AKON
akon, konvikt, (we gettin arab money swag tpain yelling we gettin arab money)
musikkkk
i got dat arab money (money)
four- star bismillahirahmanirahim
straight cash wanna keep on comin
lemme exchange da currency coz its so foreign
i got dat arab money (money) makin upto 5 kind
your minds on the money, diamond mine still runnin
on all of africa you can ask tarzan

KIITIKIO x1 (heyyyyyyyyyyyyyy)
senegal! (we gettin arab money)
senegal! (we gettin arab money)
yay!
chorus x1 (heyyyyyyyyyy)
konvikt (we gettin arab money) (alright boyz)
konvikttttt musikkk (we gettin arab money)

LIL WAYNE
khaled dar say gettin money errday
his smile look like iced out perrier
bury me a g and tell ma kids that i was
now jump into ya grave do you dig what i dug
cash money universe, my old town check
20 chains look like a scarf on my neck
young money entertainment the girls theyre fine
(and buck a motherfucka money hall of fame) (arab money)
ya!

KIITIKIO x2

Friday, October 2, 2009

MTAGWA KUWANIA UBINGWA WA WBO





BONDIA nyota wa Tanzania anayeishi Philadelphia nchini Marekani, Rogers Mtagwa anatarajiwa kupanda ulingoni Jumamosi (Oktoba 10, 2009) katika ukumbi wa Wamu Theater, Jijini New York, kuzipiga na bingwa wa WBO, Juan Manuel Lopez, akiwania taji hilo katika uzito wa Super Bantam.
Katika barua pepe aliyoituma Mtagwa kwa mwandishi wa habari hizi, amewaomba Watanzania wamuombee dua atwae taji hilo la dunia lenye pesa nyingi.
“Napigania ubingwa wa dunia wa WBO Jumamosi, napigana na bondia mmoja mkali sana, Watanzania waniombee dua nishinde, pambano hili litaonyeshwa dunia nzima, Watanzania wengine wanaweza kuliona live online (kwenye mtandao)”alisema Mtagwa.
Mtagwa anayetumia jila la utani, The Bull kwa sasa badala ya Tiger aliloingia nalo nchini humo mwaka 2000; Machi 22, mwaka huu alitimiza miaka 30 na Jumamosi atakuwa akizipiga na bondia mwenye umri wa miaka 26 tu. Hili litakuwa pambano gumu kweli kwa Mtagwa, kwani Juan ajulikanaye kama Juanma kwa jina la utani ni bondia bora na hodari haswa, mwenye rekodi nzuri kaunzia ngumi za Ridhaa.
Raia huyo wa Puerto Rico alicheza michuano mbalimbali mikubwa katika ngumi za Ridhaa ikiwemo Michezo ya Amerika ya Kati na Caribbean mwaka 2002, Michezo ya Amerika mwaka 2003 na Olimpiki mwaka 2004 na baada ya mafanikio hayo, ndipo akajitosa kwenye ndondi za kulipwa mwaka 2005.
Hakuchelewa kupata mafanikio kwenye ndondi za kupigana kifua wazi, kwani Septemba 30, mwaka 2006 alimtwanga Jose Alonso na kutwaa ubingwa wa Mabara wa WBO (Latino), uzito wa Super Bantam, kabla ya Juni 7, mwaka jana kumtandika Daniel Ponce de Leon kwa Technical Knockout (TKO) na kutwaa ubingwa wa dunia wa WBO katika uzito huo.
Mtagwa mbali na kuwa bingwa wa Baraza la Ngumi Amerika Kaskazini (NABF), pia ni bondia anayeheshimika na vyama vyote vikubwa vya ndondi duniani, WBO, WBC na IBF.
Mtagwa ambaye yupo chini ya Meneja Joe Parella na kocha Bobby ‘Boogaloo’ Watts, bondia wa zamani wa uzito wa Middle, anapigana kwa staili ya Orthodox (anapigia mkono wa kulia) atakuwa na wakati mgumu Jumamosi, kwani mpinzani wake anapigana kwa staili ya Southpaw (anapigia mkono wa kushoto). Wataalamu wa ndondi wanasema kwamba, bondia wa Orthodox ili kumpiga Southpaw, inabidi afanye kazi sana ulingoni, kama ambavyo Floyd Mayweather Jr, amekuwa akifanya.
Pamoja na kupigana kwa staili ya Orthodox, lakini Mayweather amekuwa akiwadunda mabondia wa Southpaw kutokana na ujanja wake wa kubadilisha badilisha mchezo ulingoni.
Akifanikiwa kutwaa taji hilo, Mtagwa atakuwa bondia wa kwanza kabisa Mtanzania kutwaa taji la ndondi la dunia la moja kati ya vyama vitatu vikubwa- WBC, IBF na WBO.
Rashid Matumla aliwahi kutwaa taji la WBU mwaka 1999 na akiwa na ndoto za kuwania mataji makubwa ya WBC, WBO na IBF, kampuni ya DJB Promotions iliyokuwa ikimmiliki ilimtema na huo kuwa mwanzo wa kupoteza kwake mwelekeo kwenye mchezo huo. Mbwana Matumla aliyewahi kutwaa taji la WBA International, angeweza kufika mbali naye, kama DJB ingeendelea kummiliki, lakini tangu ilipomtema, amepoteza mwelekeo pia.

Wednesday, July 22, 2009

NAKUPA LYRICS ZA MTU MZIMA SUGU...





WIMBO: Ringa:
MWIMBAJI: Sugu. Feat, Ngwair, Dr Levy

NGWAIR:
Uuuuh,Yeah, Suguu Ngwaur na Dr Levy collabo iko heavy,
yeah,Mj... I can hear u, sex mama ringa baby, yeah!
mtoto una rangi ya mvuto safi na pozi, vyako vito,
vinashaini off coz, true! mtoto matawi ya juu,
uzuri unao figa unayo usijali we ringa tuu,
mtoto unang'aa gheto mwanga wa mshumaa,
nipe zidi ya catwalk unapokrosi kwa mtaa,
ah, ah, uzuri wako wa asili akili wako utajiri
heshima hadi usafiri kuringa unastahili (ringaa),
bambataa utadhani mko wawili,
siyo siri wengi tu unawachanganya akili, (ringaa),
wala usione soo, kwani tayari tupo kwenye dancing floor,
so deep it low then bring it up slow,
unapokata machizi wote wanabaki like woo!
ha, haa, ringa tuu mamaa we kifaa japo wazushi bado wanakataa,
we ringaa...

CHORUS:
Ringa ringa ringa ringa kama unavyoringaa..
(ringaa) ringa ringa ringa baby kama unavyoringagaa...
( we ringaa) x 2


DR LEVY:
Hahaaaa! uuuh!mtoto umeumbika maridadi unanipa midadi,
ah sikusifii makusudi una thamani zaidi ya gold,
Bongo ingejivunia kama ungekuwa first lady,
siyo tu nakusifia ukweli nakwambia mamaa,
kuwa nawe binafsi najivunia, umbo lako ni la ajabu,
halijifichi hata unapovaa hijabu,
kama ungependa umiss ungeshinda,
hakuna jaji wa kupinga miss world usingedunda,
ah, ungetoa nuksi kwa mtu mzima Lundenga,
kama kawaida hupandishi mitungi kinywaji chako ni soda,
unang'ara bila poda baby, na kwa upeo mtoto mi nakupa shada,
kukumiliki ni zali nasema asante mungu,
hata shule hukufeli na unaishi kiswahili,
hupendi kabisa uzungu, ah, kwangu fahari,
we ni binti mrembo, sita kwa sita mtoto unayajua mambo,
sitaki tena shombo sitaleta mtoto wa kambo,
naogopa kukupa mimba ntatibua shepu ya tumbo,
japo kuzaa ni lazima na nataka ubaki kama pambo,
kuna watu wanachonga eti mtoto unaringa nami siwezi kupinga
nasema ruksa kuringa... wooo.

CHORUS:
Ringa ringa ringa ringa kama unavyoringaa..
(ringaa) ringa ringa ringa baby kama unavyoringagaa...
( we ringaa) x 2

SUGU:
Nimeshaona mademu kutoka kila sehemu,
una haki ya kuringa we ni bonge la demu,
mtaani ni nani asiyekufahamu,
kila time nikikuona usoni unatabasamu,
machoni kukutazama mtu mzima siishi hamu,
una maumbile matamu, na zaidi umetulia
na kichwani uko timamu,
ha, na huna mzuka wa kutaka kwenda Ulaya,
unakomaa na chuo ili baadaye uwe lawyer,
wewe siyo sister duu kanyaboya,
uzuri kama wako wengine wanautumia kwa umalaya,
napenda hata mavazi unayovaa,
napenda pozi zako kwenye kiti unapokaa,
ukisimama tumbo flati utadhani bado hujazaa,
ha, nje kimini lazima thong kwa ndani,
na gitaa la nyuzi kadhaa kiunoni,
na ndo maana nikiwa nawe mkono daima uko ndani,
na ukienda club mabitozi ni vurugu lakini wanatulia
wanapojua uko na Sugu, kwani wanajua Sugu pia ni mtu wa mavurugu...
ringaa ringaa...

CHORUS: Ringa ringa ringa ringa kama unavyoringaa..
(ringaa) ringa ringa ringa baby kama unavyoringagaa...
( we ringaa) x 2






WIMBO: Kiburi
MWIMBAJI: Sugu Feat. Stara Stara:

STARA:
Wanachotaka wewe upate tabu
Raha kidogo tu chuki bila sababu
SUGU: Najua mama, hili ntalikabili,
Kwani najua jeuri dawa yake ni kiburi

VESI LA KWANZA
Kwa wanaonijua toka enzi za Mbeya Day,
au wakati bado mdogo mama aliponiita May,
miaka chini ya kumi tu nina jina mtaani,
kila mtu alinijua mimi mtoto wa nani,
ni hivyo hivyo mpaka waalimu shuleni,
na ndo maana mpaka leo mimi sishangai kushaini,
nilipoanza muziki sikujua mafanikio yangeambatana na chuki
mara ngapi nageukwa na nnaowaita marafiki?
sasa nalala macho wanafiki siwataki,
maana kila ninachofanya wanaonekana hawataki,
Ha! na sijali wanachosema,
Baba alinifundisha kutazama mbele daima,
na moto ni ule ule tu hakuna wa kuuzima,
najua wanachotaka, kuona Sugu kachoka…
…ili wapate kucheka, watasubiri watachoka,
watapanda watashuka, mi nabaki vile vile kila siku kila mwaka,
na bado wanakilisha tu chama la Madeiwaka,
mi ni fighter nafaiti bila kuchoka...
aaaaaaaaaah aaaaaaaaaaaaaaah!

STARA:
Wanachotakaaa ooh wanavyotaka...
Wanachotaka wewe upate tabu
Raha kidogo tu chuki bila sababu


VESI LA PILI:
Kweli jeuri dawa yake ni kiburi,
na mi ntabaki mbishi mpaka nilione kaburi,
wako wapi walionicheka shuleni nilipofeli,
pilika zangu mtaani zimenifikisha mbali,
tisini na tatu niko boda naitafuta South Afrika,
leo kila nnapotaka naenda zangu Amerika,
ndivyo maisha yanavyoweza kuchenji,
leo niko na Terrano kesho VX au Range,
na bado nikiwa Bar nadai chenji, Ha,
pata picha Sugu angekuwa kisha choka,
hakika historia ingekuwa imeshafutika,
mabwana mdogo wangeongea kuhusu gemu wanavyotaka,
ningetoweka kama wastaafu wa soka,
kumbuka niliacha fani wakasema wananimiss,
nimerudi kwa kishindo wengine wanapata stress,
wanabaki tu wanasema... na, mi nasema waseme watakavyosema,
kwani watasema mchana na usiku watalala,
na wakiamka asubuhi mi naendeleza bakora, waah!

STARA:
Wanachotaka wewe upate tabu
Raha kidogo tu chuki bila sababu

VESI LA TATU
Maisha yangu yote nimepata sana tabu,
nashangaa raha kidogo tu chuki bila sababu,
sijawafanyia madhambi vipi wanataka nitubu?!
wanasema nikisema wanasema mi nna gubu,
najua bado niko juu kwenye listi,
sina mchezo na life ila siogopi kulosti,
haya siyo maisha yangu nyie mafala,
yote ni mambo tu ya hela,
siku nikikosa mchuma niko ndani ya daladala,
na hata kama ni kweli mi sikuzaliwa gheto,
nimekulia street na nimeshazoea msoto,
na enzi zangu machizi waliniita msela ngoto,
na kwa Madj sitoi rushwa za kitoto,
hata waendelee kubana hawatazuia ndoto,
au niende PCB niwapelekee za moto?
kama noma iwe noma na ikibidi ile kinoma,
wananiua kimuziki kwa nini nione huruma?

STARA:
Wanachotaka wewe upate tabu
Raha kidogo tu chuki bila sababu
Wanachotaka wewe upate tabu, raha kidogo tu chuki bila sababu,

SUGU: Najua mama hili ntalikabili kwani najua jeuri dawa yake ni kiburi
STARA: Wanachotaka wewee upate tabu raha kidogo tu chuki bila sababuAh!
SUGU: Najua mama, hili ntalikabili kwa najua jeuri dawa yake ni kiburi haaa!

WATOTO WA ILALA HAO...

Wa pili kutoka kushoto ni Irene Karugaba, mrembo kutoka Mzizima


MISS ILALA SAFARINI ARUSHA...

Mshiriki wa Miss Ilala, ambaye ni Miss Dar es Salaam (Mzizima) Glory William akitoka ndani ya hoteli ya Lamada, Ilala Jijini Dar es Salaam, kuelekea kupanda gari tayari kwa safari ya Arusha, kutembelea mbuga za wanyama.