• HABARI MPYA

    Saturday, March 24, 2012

    RAIS FIFA TAABAAN, AMELAZWA KWAO

    RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Joao Havelange bado yuko hospitali nchini Brazil akisumbuliwa na maradhi yaliyosababisha virusi fulani kwenye kifundo chake cha mguu wa kulia.
    Hospitali ya Samaritano imesema jana, babu huyo mwenye umri wa miaka 95, Havelange anapumua bila msaada wa mashine, lakini hali yake bado ipo chini ya uangalizi wa kina.
    Havelange alilazwa Jumapili, akisumbuliwa na maradhi ya kudhoofu viungo. Bao haijawekwa wazi kama maradhi hayo  yamesambaa.
    Havelange aliiongoza FIFA kuanzia mwaka 1974 hadi 1998, alipomuachia Seppe Blatter anayeendelea hadi sasa.
    Alistaafu kwenye Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki mwaka jana, kwa sababu za kiafya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS FIFA TAABAAN, AMELAZWA KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top