Tyson |
BONDIA Mike Tyson anajuta, lakini
wote tuna majuto. Kitu ambacho hawezi kujutia daima, ni kuwa bondia wa kulipwa.
Katika mahojiano na gazeti la Mirror,
Mike amezungumzia show yake ya “Undisputed Truth,” lakini akili yake ni kama
mto jinsi unavyoenda.
Kwa sababu gazeti hilo
liliandika nchini Uingereza kulaani Tyson alichofanya kabla ya pambano lake na Lennox
Lewis.
“Wakati huo napigana na Lennox
Lewis,” alisema Tyson, “Nilikuwa ovyo ile mbaya na nilikuwa nafikiri mtu angenipiga
bastola. Nilikuwa najichukia na kila kitu kilichokuwa karibu yangu.”
Hayuko ovyo tena na hajichukii
tena na yeyote aliye jirani yake. Na wakati Iron Mike yupo nje ya ulingo wa ndondi,
ndondi haziwezi kuwa mbali yake, na mtu fulani ambaye anaonekana dhahiri
amebadilika.
“Nini David Haye amefanya Munich
alipopigana (kavukavu) na Chisora,” Tyson alisema, “hiyo haikuwa nzuri. Huo ulikuwa
ni upumbavu ambao niliwahi kuufanya mara awali. Nafikiri kwamba, wakati naangalia
hiyo. Hakuna aliyewahi kufanya kama mimi katika kuvunja sheria za ngumi. Haye na
Chisora walitakiwa kupinga nilichokifanya. Angalau Haye hajawahi kumng’ata
yeyote sikio. Walichokifanya kilikuwa bure.”
Mike alipoulizwa anafikiria nini
kuhusu ndondi za uzito wa juu kwa sasa, jibu lake lilikuwa la ajabu.
“Nafikiri ndondi za uzito wa juu
ni nzuri sana kwa sasa. Akina Klitschko wanafanya babu kubwa. Si kosa lao
kwamba hakuna ushindani wa kutosha.
Lakini sikubaliani na wazo
kwamba mabondia wa leo si wazuri kama wa zamani. Kama ungemuuliza Joe Frazier
kama angeweza kunipiga wakati nilipokuwa katika kiwango cha juu enzi zangu, angesema,
‘ndio.’ Hivyo ndivyo ngumi zinavyokwenda.
“Nafikiri naweza kuwapiga
mabondia wa kizazi kijacho, lakini ukweli wa historia ni kwamba mabondia
wanakuwa bora na bora, miili mikubwa na wenye nguvu na nguvu. Nilikuwa na mwili
mkubwa kuliko Rocky Marciano na sikuwa mmoja wa mabondia wenye miili mikubwa katika
kizazi changu.”
Tyson anafahamu historia ya
ngumi, lakini hakuna hakika kama watu watakubaliana na uchambuzi wake. Lakini katika
kila maoni yake. Na Tyson, mpende usimpende, msamehe au usimsamehe, lakini
amebadilika sana tu.
0 comments:
Post a Comment