• HABARI MPYA

    Sunday, May 20, 2012

    MAFISANGO ANAZIKWA LEO

    MWILI wa kiungo wa Simba, Patrick Mutesa Mafisango unatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwao Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 
    Gazeti la serikali, Habari Leo la leo, limeandika kwamba Mafisango aliyefikwa na mauti usiku wa kuamkia Alhamis baada ya kupata ajali ya gari, mwili wake ulisafirishwa alfajiri jana kuelekea Kinshasa na kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga msafara huo ulifika salama. 
    Mwili wa mchezaji huyo kipenzi cha Wanasimba uliagwa juzi kwenye Uwanja wa TCC 
    Chang’ombe kabla ya safari ya uwanja wa ndege tayari kwenda kwenye makazi yake ya milele. 
    Nalo Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetuma salamu za 
    rambirambi kwa uongozi wa Simba, Watanzania na wapenda soka wote wa ukanda wa Afrika 
    Mashariki na Kati. 
    Katika taarifa yake jana, Katibu wa Cecafa, Nicholaus Musonye alisema Baraza lake limeshtushwa na taarifa za msiba wa Mafisango kwani ameondoka akiwa kijana mdogo. 
    “Bado wanasoka walikuwa wakiuhitaji mchango wake, alikuwa mchezaji mahiri sana 
    aliyejizolea umaarufu katika ukanda wetu huu, tulikuwa naye kwenye mashindano ya Kombe la Kagame, Kombe la Chalenji, lakini tumuombee tu afike salama,” alisema. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAFISANGO ANAZIKWA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top