• HABARI MPYA

    Sunday, May 06, 2012

    MCHAKATO TUZO ZA WANAMICHEZO BORA WAANZA


    CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimeanza mchakato wa Tuzo kwa Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2011.
    Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando (pichani kushoto) ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba kama ilivyokuwa mwaka uliopita Kamati ya Utendaji ya TASWA imeamua suala la mchakato wa kuwapata wanamichezo hao lifanywe na kamati maalum nje ya Kamati ya Utendaji ya TASWA lengo ikiwa ni kupanua wigo na kuwashirikisha wadau wengi zaidi katika jambo hili nyeti.
    Kutokana na hali hiyo Kamati ya Utendaji ya TASWA imeshateua kamati maalum ya kusimamia tuzo hiyo, ambapo kamati hiyo ambayo tayari imeshaanza vikao vyake jijini Dar es Salaam ipo chini ya Mhariri Mkuu wa gazeti la Spoti Starehe, Masoud Sanani, ambaye pia aliiongoza kamati hiyo mwaka uliopita.
    Kamati hiyo ya Tuzo ilikutana mara ya mwisho hivi karibuni kwa ajili ya kupanga namna ya kuendesha tuzo hizo kwa mwaka huu ili iwe bora zaidi ya ilivyokuwa mwaka jana.
    Pamoja na mambo mengine kamati ilikubaliana vyama vya michezo vishirikishwe kwa kuviandikia barua ili vitume majina ya wanamichezo wao waliofanya vizuri kwa mwaka 2011.
    Kutokana na hali hiyo kila chama cha michezo kitawasilisha  kwa kamati majina matatu ya wanamichezo wake waliofanya vizuri mwaka jana kwa wanaume matatu na wanawake matatu, ambao mmojawao atakuwa ndiye mshindi wa mchezo husika kwa mwaka jana.
    Pia kila mshindi miongoni mwa wanamichezo hao atashiriki kuwania tuzo ya Mwanamichezo wa Bora wa Mwaka 2011. Tarehe na mahali ambapo tuzo itafanyika itatangazwa wiki hii baada ya kumalizika vikao muhimu, ambapo pia mdhamini wa tuzo atatajwa, ingawa TASWA inafungua mlango kwa kampuni zaidi zijitokeze kudhamini kwa vile tuzo ya mwaka huu itakuwa ya aina yake.
    Kwa hiyo wafuatao ndio wanaunda Kamati ya TASWA ya Kusimamia Upatikanaji wa Wanamichezo Bora wa Tanzania kwa mwaka 2011, wengi wakiwa ni wale waliokuwepo mwaka uliopita..
    Mwenyekiti wa Kamati atakuwa Sanan, ambaye ni Mhariri wa gazeti la Spotistarehe, Katibu wa kamati atakuwa Amir Mhando ambaye ni Katibu Mkuu wa TASWA,  Mshauri wa Kamati atakuwa Juliana Yassoda ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo. Pia Kamati itaomba Ofisa mmoja wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) naye kuwa mshauri wa kamati.

    Orodha kamili ya wajumbe ni
    1.Amour Hassan-Mhariri Nipashe
    2. Rashid Zahoro-Mhariri gazeti la Burudani
    3. Alex Luambano-Clouds FM
    4. Tulo Chambo-Mhariri Tanzania Daima
    5. Mbonile Burton-HabariLeo
    6. Chacha Maginga-TBC1
    7.Frank Sanga-Mhariri Mwanaspoti
    8. Michael Maurus-Super Star
    9. James Range-Star TV
    10.Editha Mayemba-Radio Tumaini
    11. Said Kilumanga-Chanel Ten/Magic Radio
    12.Rehule Nyaulawa-Mkurugenzi Times FM
    13. Angel Akilimali-Meneja Vipindi Radio Uhuru
    14. Masoud Sanan-Mhariri Spotistarehe
    15. Amir Mhando-Katibu Mkuu TASWA
    16. George John –Katibu Msiadizi TASWA
    17.Patrick Nyembela-EATV
    18: Juliana Yassoda-Naibu Mkurugenzi Idara ya Michezo
    19. Luqman Maloto-Championi
    20. Deo Rweyunga-Radio One
    21. Andrew Kingamkono-Mhariri Mwananchi
    22. Dominick Isiji-The African
    23. Ofisa kutoka BMT
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MCHAKATO TUZO ZA WANAMICHEZO BORA WAANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top