• HABARI MPYA

    Wednesday, July 11, 2012

    OKWI ATUA AUSTRIA KUFANYA MAJARIBIO

    Okwi
    Na Mahmoud Zubeiry
    MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi, ameikosesha klabu yake Sh. Bilioni 2 kwa kukataa kujiunga na klabu ya Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini, kwa kutimikia nchini Austria badala ya Italia kama ilivyodai ana ofa ya kufanya majaribio na klabu ya Parma.
    Okwi hivi sasa yuko Austria anafanya majaribio katika klabu ambayo iko tayari kutoa Euro 600,000 akifuzu na si Italia kama ilivyoelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ wiki mbili zilizopita.
    Uchunguzi wa kina uliofanywa na BIN ZUBEIRY umegundua Okwi aliondoka mwishoni mwa wiki Uganda kwenda Austria na hadi mwishoni mwa wiki hii tayari itajulikana kama amefuzu au la.
    Awali Olando Pirates ya Afrika Kusini ilimuomba Okwi akafanye majaribio huko kama angefuzu wangemsajili dau la dola 550,000 kabla ya kuibuka kwa taarifa za kutakiwa Italia na klabu ya Parma.
    Hata hivyo, Simba SC ilisema imeshindwa kumshawishi Okwi kwenda kucheza Afrika Kusini kwa kuwa mwenyewe anataka kucheza Ulaya tu. Wakala aliyeiunganisha Simba na Pirates akawasilisha ofa nyingine kutoka Mamelodi, ambayo ni Euro 600,000 na kupanda hadi Sh. Bilioni 2, lakini bado mabingwa hao wa Tanzania, walishindwa kumshawishi Okwi kwenda Ligi Kuu ya Afika Kusini (PSL).
    Akiwa Austria, bado Sundown wanamfuatilia Okwi na leo ndio wameambiwa Okwi yupo nchi hiyo ya Ulaya.
    Wasiwasi uliopo ni kwamba Okwi anaweza kukwama Austria na kuigeukia ofa ya Mamelodi wakati dirisha la usajili limefungwa, au Mamelodi tayari imepata mchezaji mwingine wa aina yake na kufunga milango.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OKWI ATUA AUSTRIA KUFANYA MAJARIBIO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top