Paschal Ochieng |
Na Mahmoud Zubeiry
SIMBA SC imevunja
mkataba na kiungo Kanu Mbivayanga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
na mshambuliaji mzalendo Danny Mrwanda na kusajili wachezaji wawili wengine wa
kigeni, beki Paschal Ochieng na mshambuliaji Daniel Akuffo kutoka Ivory Coast.
Mshambuliaji kutoka Hearts Of Oak ya Ghana tayari yupo Dar es Salaam tangu saa 3:00 asubuhi na jioni ya leo
atakwenda kuungana na kikosi cha Simba kilichopo kambini Arusha, wakati Ochieng
kutoka AFC Leopard ya Kenya tayari mtu amekwenda kumpokea mpakani, Namanga.
Kwa maana hiyo, Simba
sasa inakuwa na wachezaji wa kigeni watano, baada ya Waganda Emmanuel Okwi, Mussa
Mudde na Mzambia Felix Sunzu.
Habari za ndani kutoka
Simba SC, ambazo zimeifikia BIN
ZUBEIRY zimesema kwamba marekebisho hayo ya usajili yanatokana na
ushauri wa Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Profesa Milovan Cirkovick, raia wa Serbia.
Cirkovck ameamua
kumuondoa kwenye kikosi chake Mrwanda, kwa sababu amempata Mrisho Ngassa na
Kanu ametemwa kwa sababu timu ina viungo wengi, hivyo ameona bora kuongeza beki
mmoja na mshambuliaji.
Wakati huo huo, kiungo
Kiggi Makassy aliyesajiliwa kutoka Yanga, sasa anahamishiwa kwenye nafasi ya
beki ya kushoto akagombee namba na Amir Maftah na Paul Ngalema.
Beki wa kulia, Haruna Shamte
ana asilimia sawa za kubaki au kutemwa kwenye kikosi cha Simba, kwani Cirkovick
anaona bora kuwatumia wachezaji wa Simba B, ambao wanafanya vizuri na wapo hadi
timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes.
Katika beki ya kati,
baada ya kumpata Ochieng, Milovan anaamini akiungana na Juma
Nyosso, Shomary Kapombe
na Obadia Mungusa atakuwa ana ukuta umara.
Lakini Milovan anataka
kuangalia hali ya timu hadi Desemba na kama ataona kuna haja ya kurekebisha
tena kikosi kabla ya kuingia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, atafanya
hivyo.
Mrwanda alisajiliwa Simba kwa ajili ya msimu ujao, akitokea Vietnam alipokuwa akicheza soka ya kulipwa sawa na Kanu aliyesajiliwa kutoka DRC. Wakati Mrwanda anasajiliwa Simba, na Yanga pia walikuwa wanamtaka, lakini Wekundu wa Msimbazi wakawazidi dau wapinzani wao wa jadi.
Mrwanda alisajiliwa Simba kwa ajili ya msimu ujao, akitokea Vietnam alipokuwa akicheza soka ya kulipwa sawa na Kanu aliyesajiliwa kutoka DRC. Wakati Mrwanda anasajiliwa Simba, na Yanga pia walikuwa wanamtaka, lakini Wekundu wa Msimbazi wakawazidi dau wapinzani wao wa jadi.
Aidha, Simba
inamsajili Ochieng kuchukuan nafasi ya Mbuyu Twite kutoka APR, ambaye alisaini
kwa Wekundu hao wa Msimbazi, baadaye akaghairi na kwenda Yanga.
0 comments:
Post a Comment