Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya


NANI HANA MASHARTI KWENDA URUSI

WINGA wa Manchester United, Nani, mwenye umri wa miaka 25, ana nia ya kuhamia Zenit St Petersburg ya Urusi bila kujali mshahara.
Beki wa Chelsea na England, Ashley Cole, mwenye umri wa miaka 31, anajiandaa kwenda Paris St Germain ya Ufaransa Januari au mwishoni mwa msimu.
Nani
Winga Mreno, Nani hajasaini mkataba mpya Manchester United
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho anaamini historia ya klabu hiyo itatosha kumshawishi mshambuliaji Mreno mwenzake, Cristiano Ronaldo, mwenhye umri wa miaka 27 kubaki, licha ya kutakiwa na matajiri wa Manchester City.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anataka mabeki Bacary Sagna, mwenye umri wa miaka 29 na Kieran Gibbs, mwenye miaka 22, kusaini mkataba mpya.
Mshambuliaji wa Colombia, Radamel Falcao, mwenye umri wa miaka 26, amekanusha taarifa kwamba ataondoka Atletico Madrid kuhamia Ligi Kuu ya England katika klabu za Manchester City au Chelsea.
Beki wa Everton, Leighton Baines, mwenye umri wa miaka 27, amechanganyikiwa mno na Manchester United kushindwa kumsajili katika usajili uliopita.

GERRARD AOTA ENGLAND BINGWA WA KOMBE LA DUNIA BRAZIL MWAKA 2014 

Nahodha Steven Gerrard, mwenye umri wa miaka 32, anafikiri England itatwaa Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka 2014.
Mshambuliaji wa Manchester United, Shinji Kagawa alitolewa nje wakati wa mapumziko katika mchezo wa kirafiki wa timu yake ya taifa, Japan dhidi ya Falme za Kiarabu (UAE) na kocha Alberto Zaccheroni.

AVB ILIKUWA ATUE BURNLEY 

Kocha wa Tottenham, Andre Villas-Boas ilibaki kidogo awe kocha Burnley mwaka 2010, lakini mkuu wa Turf Moor hakuelewa mipango yake, kiitabu kipya kimefichua siri hiyo.