• HABARI MPYA

    Saturday, September 15, 2012

    SIMBA YAUA 3-0, AZAM YASHINDA 1-0, YANGA YATOLEWA KAPA SOKOINE

    Akuffo akishangilia bao lake


    Akuffo akishangilia huku akifuatwa na Juma Nyosso kupongezwa

    Nassor Masoud 'Chollo' anatia krosi 

    Chollo anatia krosi

    Okwi anashangilia bao lake 

    Ngassa akishangilia baada ya pasi yake kutumbukizwa kimiani na Chollo

    Wachezaji wa Simba wakimpongeza Ngassa (16) kwa kutoa pasi ya bao la pili. Kushoto kabisa ni mfungaji wa bao hilo Chollo akimuwahi kumpongeza 

    Okwi anapasua

    Kikosi cha Lyon leo

    Kikosi cha Simba leo
    Na Mahmoud Zubeiry

    SIMBA SC imeanza vema kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, jioni hii baada ya kuichapa mabao 3-0 African Lyon katika mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na Emanuel Okwi dakika ya 33 baada ya kuwatoka mabeki wa Lyon na Nassor Masoud ‘Chollo’ dakika ya 36 akiunganisha krosi ya Mrisho Ngassa.
    Lyon walikosa penalti dakika ya 35, baada ya mkwaju wa Sunday Bakari kupanguliwa na Juma Kaseja, kufuatia Mwinyi Kazimoto kuunawa mpira kwenye eneo la hatari. 
    Kipindi cha pili, Lyon kidogo walirekebisha makosa yao, lakini bado Simba iliendelea kutawala mchezo na dakika ya 56, Danniel Akuffo aliifungia timu yake bao la kuhitimisha ushindi kwa mkwaju wa penalti, baada ya Emmanuel Okwi kuangushwa kwenye eneo la hatari.
    Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi ‘Boban’, Daniel Akuffo/Ramadhan Chombo, Mrisho Ngassa/Abdallah Juma na Emanuel Okwi.
    African Lyon; Abdul Seif, Johanes Kajuna, Hamadi Manzi, Sunday Bakari, Benedictor Mwamlangala, Sunday Hinju, Obina Salamusasa, Semmy Kessy, Iddi Mbaga, Jacob massawe na Yussuf Mlipili.
    Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Yanga imelazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.    
    Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Hamisi Kiiza, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Nizar Khalfan/Athumani Iddi, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Didier Kavumbangu/Simon Msuva na Stefano Mwasyika.
    Kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, bao pekee la Abdulhalim Humud liliipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.
    Azam FC; Deo Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Abdulhalim Humud, Ibrahim Mwaipopo, Himid Mao/Jabir Aziz, John Bocco, Abdi Kassim/Kipre Balou na Kipre Herman Tchetche.
    Kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, bao pekee la kiungo Mkenya, Jerry Santo dakika ya 41 liliipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya Mgambo FC.
    Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, wenyeji Polisi wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar ya Turiani, Manungu.
    Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Toto Africans imelazimishwa sare ya 1-1 na JKT Oljoro, wakati Uwanja wa Chamazi, Mbagala, JKT Ruvu imeifunga Ruvu Shooting mabao 2-1.

    MATOKEO MECHI ZOTE LIGI KUU LEO

    Simba                 3-0      African Lyon

    Kagera Sugar     0-1      Azam FC

    Prisons               0-0      Yanga

    Coastal Union     1-0      Mgambo JKT

    Toto African        1-1      JKT Oljoro

    Polisi Moro          0-0      Mtibwa Sugar
    JKT Ruvu            2-1      Ruvu Shooting 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YAUA 3-0, AZAM YASHINDA 1-0, YANGA YATOLEWA KAPA SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top