• HABARI MPYA

    Wednesday, October 17, 2012

    MANJI AENDA KUFANYA IBADA YA HIJJA


    Yussuf Mehboob Manji, Alhaj mtarajiwa 

    Na Mahmoud Zubeiry
    MWENYEKITI wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Yussuf Mehboob Manji kesho anatarajiwa kwenda Makka, Saudia Arabia kufanya ibada ya Hijja.
    Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka kwa mtu aliye karibu na Manji zimesema kwamba, Manji ameamua kwenda kufanya ibada hiyo ya Hijja kufuata asili ya ukoo wao, wote waislamu safi.
    Ibada ya Hijja inatararajiwa kufanyika wiki ijayo Makka na kundi la mwisho la waumini wa dini ya Kiislamu litakalokwenda huko, linatarajiwa kuondoka kesho.
    Akikamilisha ibada ya Hijja, Manji atakuwa sawa na Mwenyekiti wa wapinzani wake wa jadi, Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage, ambaye alikwenda kufanya ibada hiyo mwaka 1999 kwa ofa wakati huo akiwa bado Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Tanzania (TFF), sasa shirikisho (TFF).
    Manji amekuwa mfadhili wa Yanga tangu mwaka 2006, wakati klabu hiyo ikiwa chini ya Mwenyekiti, Francis Mponjoli Kifukwe na baada ya kuona jitihada zake za kuifanya Yanga iwe ya hadhi ya juu zinakwamishwa na viongozi, Julai 14, mwaka huu akaamua kujitosa kugombea Uenyekiti wa klabu hiyo, katika uchaguzi mdogo.
    Ni miongoni mwa wafanyabiashara vijana wenye mafanikio makubwa, ambaye amerithi na kuendeleza vema utajiri wa baba yake, marehemu Mehboob Manji. 
    Ibada ya Hijja ipo katika nguzo ya tano ya Uislamu; inayomtaka muumini wa dini ya Kiislamu mwenye uwezo kwenda kuitekeleza ibada hiyo na kuna imani kwamba baada ya ibada hiyo, muumini huyo hufutiwa dhambi zake za awali ila baada ya hapo, hatakiwi tena kurudia kufanya yaliyokatazwa na mafundisho ya dini hiyo na akifanya hivyo 'atajipalilia makaa ya moto' siku ya hukumu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MANJI AENDA KUFANYA IBADA YA HIJJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top