• HABARI MPYA

    Thursday, November 08, 2012

    FILAMU YA SHUJAA KUMPONGEZA RAIS KIKWETE KUZINDULIWA DESEMBA

    Mtayarishaji wa filamu mpya iitwayo Shujaa, Adam Kasale akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dar es Salaam asubuhi ya leo kuhusu ‘picha hilo’ ambalo limetayarishwa katika kiwango cha juu cha ubora. 

    Mwigizaji wa filamu hiyo, Henry Babuu kushoto na Barbra Kalugira kulia, Meneja Masoko na Mratibu wa filamu hiyo

    Isakwisa Kanyenyela kushoto na Adam Semkwiji ‘Snare’ na Innocent Nyika, waliohusika katika idara za kitaalamu kwenye kutayarisha filamu hiyo.

    Na Princess Asia
    KAMPUNI ya Afronode Films, imeandaa filamu maalum iliyopachikwa jina la Shujaa ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kitwete kwa kuhamasisha wananchi kupima ukimwi kwa hiyari.
    Akizungumza mjini Dar es salaam leo, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Barbra Kalugira, alisema kuwa kila kitu kimekamlika ambapo uzinduzi wake utafanyika Desemba mosi ambayo ni siku ukimwi duniani.
    Kalugira alisema kuwa katika filamu hiyo itazungumzia watu kwenda kupima kwa hiyari kama alivyofanya Rais wa Tanzania ambaye ndiye kiongozi pekee katika ukanda wa Afrika kuhamasisha kupima ukimwi.
    "Ni kitendo cha kumpongeza sana Rais wetu kwa kwenda kupima kwa hiyari na kuhamasisha wananchi wote wajitokeze kupima hivyo tunazindua filamu hiyo ambayo inazungumzia janga la ukimwi na madhara ya kutopima"alisema Kalugira.
    Pia Kalugira alisema kuwa katika filamu hiyo itamzungumzia kijana mmoja ambaye alikataa kwenda kupima alipokutana na msichama ambaye ni muadhirika wa ukimwi.
    Alisema mpaka kukamilika kwa filamu hiyo jumla ya sh.milioni 35 zimetumika katika kukamilisha.
    Kalugira alisema kuwa mpaka wiki ijayo watakuwa wamejua ni wapi watafanya uzinduzi huo.
    "Filamu yetu inaitwa Shujaa ambayo tutazindua Desemba Mosi (2012), lakini bado hatujajua ni wapi tutafanyia uzinduzi huo ambao unaujumbe mkubwa kwa jamii kuhusiana na janga zima la Ukimwi"alisema Kalugira.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: FILAMU YA SHUJAA KUMPONGEZA RAIS KIKWETE KUZINDULIWA DESEMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top