• HABARI MPYA

    Sunday, November 18, 2012

    HAYATOU KUFUNGUA TUSKER CHALLENGE WIKI IJAYO

    Hayatou kushoto akiwa na Rais wa FIFA, Sepp Blatter kulia

    Na Mahmoud Zubeiry
    RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou amekubali kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Cecafa-Tusker Challenge wiki ijayo mjini Kampala, Uganda.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Rogers Mulindwa ameiambia BIN ZUBEIRY leo kutoka Uganda kwamba, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) tayari limepokea uthibitisho wa Hayatou kufungua michuano hiyo kutoka makao makuu ya CAF, Cairo, Misri.
    Bosi huyo wa soka barani, anatarajiwa kuwasili Kampala Novemba 22, kufuatia mwaliko huo wa Rais wa CECAFA, Leodegar Tenga.
    Rais wa FUFA, Lawrence Mulindwa amesema Uganda imefurahia heshima hiyo ya ujio wa Hayatou, ambaye atafuatana na viongozi mbalimbali wa CAF, akiwemo Katibu Mkuu, Hicham El Amrani, Mohamed Raouraoua, Constant Omari na Ngangue Appolinaire. Katika ziara yake hito, Hayatou atahudhuria Mkutano wa CECAFA katiuka hoteli ya Serena Ijumaa ya Novemba 23 kabla ya kufungua rasmi michuano ya mwaka huu ya Cecafa-Tusker Cup Uwanja wa Namboole jioni ya siku inayofuata.
    Uganda itawakaribisha jirani zao Kenya katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo saa 10:00 jioni, Jumamosi ya Novemba 24.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: HAYATOU KUFUNGUA TUSKER CHALLENGE WIKI IJAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top