// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ZANZIBAR KUJARIBU BAHATI TENA LEO TUSKER CHALLENGE, KUKIPIGA NA RWANDA NI VITA YA NIYONZIMA NA CANNAVARO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ZANZIBAR KUJARIBU BAHATI TENA LEO TUSKER CHALLENGE, KUKIPIGA NA RWANDA NI VITA YA NIYONZIMA NA CANNAVARO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Thursday, November 29, 2012

        ZANZIBAR KUJARIBU BAHATI TENA LEO TUSKER CHALLENGE, KUKIPIGA NA RWANDA NI VITA YA NIYONZIMA NA CANNAVARO

        Zanzibar Heroes

        Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
        MASHUJAA wa visiwani, Zanzibar Heroes leo wanatupa kete yao ya pili katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwa kumenyana na Rwanda katika mchezo wa Kundi C, utakaoanza saa 12:00 jioni Uwanja wa Mandela, Namboole, mjini hapa.
        Mchezo huo utatanguliwa na mchezo mwingine, kati ya Malawi na Eritrea ambao utaanza saa 10:00 jioni kwenye Uwanja huo.
        Zanzibar walilazimishwa sare ya bila kufungana na Eritrea katika mchezo wa kwanza, wakati Malawi ilifungwa mabao 2-0 na Rwanda.
        Zanzibar wanahitaji kushinda mechi ya leo, ili kuweka hai matumaini ya kuingia Robo Fainali ya michuano hii, ingawa mbele ya Rwanda huo utakuwa mtihani mgumu kwao.
        Moja kati ya burudani zinazotarajiwa kwenye mechi hiyo ni kushuhudia wachezaji wawili wa klabu moja, Yanga SC ya Dar es Salaam, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Zanzibar na kiungo Haruna Niyonzima wa Rwanda, wakichuana leo, tena wote wakiwa manahodha wa timu zao za taifa.
        Baada ya sare katika mechi ya kwanza, Cannavaro pamoja na kuwaomba radhi Wazanzibari kwa sare hiyo, lakini pia ameahidi watajituma na kufanya vizuri katika mechi zijazo. 

        MECHI ZILIZOSALIA:
        RATIB KUNDI A:
        Novemba 30, 2012:
        Kenya v Ethiopia                  (Saa 9:00 Alasiri)
        Sudan Kusini v Uganda       (Saa 12:00 jioni)
        RATIBA KUNDI B:
        Desemba 1, 2012:
        Sudan v Burundi                 (Saa 9:00 Alasiri)
        Somalia v Tanzania             (Saa 12:00 jioni)
        RATIBA KUNDI C:
        Novemba 29, 2012:
        Malawi v Eritrea                   (Saa 9:00 Alasiri)
        Rwanda v Zanzibar             (Saa 12:00 jioni)
        Desemba 2, 2012:
        Malawi v Zanzibar               (Saa 9:00 Alasiri)
        Eritrea v Rwanda                (Saa 12:00 jioni)

        MSIMAMO KUNDI A:
                              P   W  D   L    GF GA GD Pts
        Uganda          2    2    0    0    2    0    2    6
        Kenya             2    1    0    1    2    1    1    3
        Ethiopia          2    1    0    1    1    1    0    3
        Sudan Kusini  2    0    0    2    0    3    -3  0

        MSIMAMO KUNDI B:
                             P   W  D   L    GF GA GD Pts
        Burundi         2    2    0    0    6    1    5    6
        Tanzania       2    1    0    1    2    1    1    3
        Sudan           2    1    0    1    1    2    -1  3
        Somalia         2    0    0    2    1    6    -5  0

        MSIMAMO KUNDI C:
                              P   W  D   L    GF GA GD Pts
        Rwanda         1    1    0    0    2    0    2    3
        Eritrea            1    0    1    0    0    0    0    1
        Zanzibar         1    0    1    0    0    0    0    1
        Malawi            1    0    0    1    0    2    -2  0

        VIWANGO VYA UBORA FIFA
        NCHI                 NAFASI
        Uganda             86
        Malawi              101
        Ethiopia            102
        Sudan               102
        Rwanda             122
        Burundi             128
        Kenya                130
        Tanzania           134
        Zanzibar            134
        Somalia             193
        Eritrea               192
        Sudan Kusini     200
        (Viwango hivi vimetoka mwezi huu)
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments
        Item Reviewed: ZANZIBAR KUJARIBU BAHATI TENA LEO TUSKER CHALLENGE, KUKIPIGA NA RWANDA NI VITA YA NIYONZIMA NA CANNAVARO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry