• HABARI MPYA

    Thursday, December 06, 2012

    SELEMBE AWAPA MALARIA + WAKENYA, TAZAMA REKODI YA HARAMBEE NA HEROES TANGU 1977

    Kikosi cha Zanzibar, Selembe wa kwanza kushoto walioinama, kiboko ya Wakenya 

    Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
    KIUNGO wa Zanzibar, Suleiman Kassim ‘Selembe‘ ndiye mchezaji ambaye anawatia hofu mno Wakenya kuelekea mchezo wa leo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole, mjini hapa.
    Mashabiki wa soka wa Kenya waliopo hapa na baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka nchini humo, wamekuwa wakimzungumzia Selembe kama mchezaji hatari na aliyebeba hatima yao leo.  
    “Selembe, yule mchezaji yupo kama Fellaini (Marouane) ni hatari sana yule, kwa kweli amebeba hatima yetu, tukiweza kumbana yule, Zanzibar wala hawafurukuti,”alisema mmoja wa mashabiki wa Kenya juzi mjini hapa, akimfananisha kiungo huyo na kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye asili ya Morocco, anayechezea Everton ya England.
    Kenya na Zanzibar zinamenyana katika Nusu Fainali ya kwanza kwenye Uwanja wa Mandela leo, mchezo ambao utafuatiwa na mechi nyingine kati ya Uganda na Tanzania Bara.
    Kenya wanaonekana kuihofia mno Zanzibar kiasi cha kuthubutu kuwarejesha kambini wachezaji wake wawili iliyowarudisha nyumbani kwa utovu wa nidhamu, Paul Were na Kevin Omondi.
    Baada ya kuifunga 1-0 Sudan Kusini katika mchezo wa pili wa Kundi A, wachezaji hao walikwenda kujirusha kwenye klabu ya usiku na kurejea kambini na wanawake, jambo ambalo lilifanya asubuhi yake wapandishwe ndege wote kurejea Nairobi, lakini kutokana na mchecheto wa mechi ya kesho, wamerejeshwa.
    Kocha wa Harambee Stars, James Nandwa aliliomba Shirikisho la Soka Kenya (FKF) liliwarejeshe wachezaji hao kwa ajili ya Nusu Fainali.
    Kocha wa Fisa FC, Charles ‘Korea’ Omondi, ambaye amekuwa akifanya mazoezi na wachezaji hao tangu warejeshwe nyumbani, amethibitisha wamebadilika kinidhamu na wako vizuri kimchezo.
    Were na Omondi wapo kwa mkopo AFC Leopards na Gor Mahia kutoka timu inayoshiriki Ligi ya Jimbo la Nairobi, Fisa FC.
    Mara ya kwanza na ya mwisho timu hizi kukutana katika hatua ya mtoano ilikuwa ni mwaka 1979 nchini Kenya, katika Nusu Fainali na wenyeji walishinda 2-0 Novemba 14 Uwanja wa Nyayo, Nairobi na mara zote zimekuwa zikikutana katika hatua ya makundi.
    Na mara ya mwisho kabisa kukutana katika mashindano haya timu hizi ilikuwa ni mwaka 1996 nchini Sudan na Kenya ilishinda 1-0.
    Kwa ujumla, timu hizi zimekutana mara 11 tangu kuanzishwa rasmi kwa michuano ya Challenge mwaka 1974 na Kenya imeshinda mechi saba, sare tatu na imefungwa moja. Kenya imeifunga Zanzibar jumla ya mabao 17, wakati yenyewe imefungwa saba.
                     
    REKODI YA KENYA NA ZANZIBAR CHALLENGE
                       P    W  D   L    GF GA Pts
    Kenya         11   7    3    1    17 7    24
    Zanzibar     11   1    3    7    7   17   6

    REKODI YA KENYA NA ZANZIBAR TANGU 1977:
    Novemba 24, 1996; Sudan Kundi B
    Kenya 1-0 Zanzibar
    Novemba 27,  1995; Uganda Kundi A
    Kenya 2-0 Zanzibar
    Novemba 30, 1991; Kundi B Uganda
    Kenya 3-2 Zanzibar
    Desemba 6, 1989; Kundi B Kenya 
    Zanzibar 0-0 Kenya B
    Desemba 14, 1987; Kundi A Ethiopia
    Kenya 0-0 Zanzibar
    Desemba 6, 1984; Kundi B Uganda
    Kenya 1-0 Zanzibar
    Novemba 21, 1982; Kundi B Uganda
    Kenya 2-2 Zanzibar
    Novemba 17, 1981; Kundi A Tanzania
    Kenya 2-1 Zanzibar
    Novemba 22, 1980; Kundi B Sudan
    Kenya 1-2 Zanzibar
    Novemba 14, 1979; Nusu Fainali Kenya  
    Kenya 2-0 Zanzibar
    Desemba 2, 1977; Kundi A Somalia
    Kenya 3-0 Zanzibar
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SELEMBE AWAPA MALARIA + WAKENYA, TAZAMA REKODI YA HARAMBEE NA HEROES TANGU 1977 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top