• HABARI MPYA

    Wednesday, April 10, 2013

    RONALDO AIPELEKA REAL NUSU FAINALI ULAYA, ILA DROGBA, SNEIJDER BADO MOTO


    WABABE wa Hispania, Real Madrid wamefuzu kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya jana usiku kufungwa 3-2 Galatasaray nchini Uturuki katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali.
    Kwa matokeo hayo, kikosi cha Jose Mourinho kimesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-2, baada awali kushinda 3-0 katika mchezo wa kwanza nchini Hispania.
    Jana Cristiano Ronaldo alikuwa wa kwanza kufunga bao dakika ya saba, lakini Emmanuel Eboue akaisawazishia Gala dakika ya 57, kabla Wesley Sneijder hajawafungia wenyeji bao la pili dakika ya 70.
    Life in the old Drog yet: Didier Drogba was among the scorers as Galatasaray won the second leg
    Utu uzima dawa: Didier Drogba alikuwa mmoja wa wafungaji wa mabao ya Galatasaray jana

    Dakika mbili baadaye, Did Drogba akafunga bao la tatu, kabla ya Ronaldo kufunga tena dakika ya 90 na kuiweka sawa barabarani Real katika mbio zake za kukimbilia taji la 10 Ulaya.
    Katika mchezo huo, kikosi cha Galatasaray kilikuwa: Muslera, Eboue/Elmander dk80, Zan, Kaya, Riera, Altintop/Amrabat dk46, Felipe Melo, Inan, Sneijder, Bulut /Sarioglu dk63 na Drogba.
    Real Madrid: Diego Lopez, Essien/Arbeloa dk31, Pepe, Varane, Fabio Coentrao, Khedira, Modric, Di Maria, Ozil/ Albiol dk81, Ronaldo na Higuain/Benzema dk73.
    Keeping the dream alive: Drogba celebrates after making it 3-1 on the night

    Shangwe za bao: Drogba akishangilia baada ya kufunga bao la tatu
    It all started so well: Ronaldo celebrates putting Real 1-0 up on the night
    Ronaldo akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza
    Back in the game: Emmanuel Eboue scored to make it 1-1
    Drogba akimpongeza ndugu yake, Emmanuel Eboue kuisawazishia Gala jana
    Ahead on the night: Galatasaray's Wesley Sneijder puts his side ahead on the night
    Wesley Sneijder akishangilia bao lake
    The comeback is on: Sneijder gives his side hope
    That should do it: Ronaldo scores at the death to secure Real's passage
    Ronaldo akishangilia bao lake la pili jana
    Into the semi: Real Madrid's Jose Mourinho shakes hands with Fatih Terim after the game
    Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho akipeana mikono na kocha wa Gala, Fatih Terim baada ya mechi

    Katika mchezo mwingine jana, Borussia Dortmund ilifanikiwa kushinda 3-0 dhidi ya Malaga kwenye Uwanja wa Signal Iduna Park, hivyo kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-2, baada ya awali kufungwa 2-0 Hispania.
    Back from the brink: Borussia Dortmund completed a stunning comeback with two goals in injury time
    Borussia Dortmund wakishangilia ushindi wao jana
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: RONALDO AIPELEKA REAL NUSU FAINALI ULAYA, ILA DROGBA, SNEIJDER BADO MOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top