• HABARI MPYA

    Friday, April 12, 2013

    TORRES AIPELEKA CHELSEA NUSU FAINALI ULAYA, SPURS NA NEWCASTLE NJE


    MATOKEO YOTE EUROPA LEAGUE JANA: (Gonga usome chini)


    KOCHA Andre Villas-Boas amewaita wachezaji wa timu yake ‘mashujaa’ usiku wa jana baada ya kutolewa kwa mikwaju ya penalti 4-1 baada ya sare ya 2-2 ndania ya dakika 120 iliyofanya sare ya jumla ya 4-4 katika Europa League dhidi ya wenyeji Basle. 
    Ulikuwa ni mkwaju wa penalti wa Marcelo Diaz’ ulioipeleka Basle Nusu Fainali katika mechi yao ya 19 ya mashindano yaliyoanza Julai mwaka jana. Lakini ilikuwa zaidi ya ajabu kwa Tom Huddlestone na Emmanuel Adebayor wote kukosa penalti zao. 
    Clint Dempsey aliifungia Spurs mabao mawili katika dakika za 23 na 82, lakini Mohamed Salah akafunga dakika ya 27 na Aleksandar 49 na kufanya sare ya 2-2. 
    Spurs iliwakosa Gareth Bale, Aaron Lennon, Jermain Defoe na William Gallas katika mchezo huo waliokuwa wakisaka ushindi wa kwanza ugenini Ulaya dhidi ya timu ambayo haikuwa imefungwa hata bao moja nyumbani tangu Oktoba. Kadi nyekundu ya moja kwa moja aliyopewa Jan Vertonghen pia iliigharimu Tottenham, ingawa Spurs pamoja na yote haijashinda mikwaju ya penalti tangu mwaka 1994. 
    Katika mikwaju ya penalti, Schar alianza kufunga, Huddlestone akakosa, Streller akafunga (2-0), Sigurdsson akafunga (2-1), Fabian Frei akafunga (3-1), Adebayor akakosa (3-1) na Diaz akamaliza kwa kufunga pia (4-1).

    Kikosi cha Basle kilikuwa: Sommer, Philipp Degen, Schar, Dragovic, Park, El-Nenny, Fabian Frei, Die/Diaz dk58, Salah/Alexander Frei dk111, Stocker/Steinhofer dk70 na Streller. 
    Tottenham: Friedel, Walker, Dawson, Vertonghen, Naughton/Assou-Ekotto dk78, Dembele/Carroll dk59, Parker/Huddlestone dk77, Holtby, Dempsey, Sigurdsson na Adebayor. 


    Down and out: Spurs look on as Emmanuel Adebayor misses from the spot
    Nje: Spurs wakimuangalia Emmanuel Adebayor akikosa penalti

    Katika mchezo mwingine, kocha Rafa Benitez alitoka uwanjani kwa furaha usiku wa jana alipoiwezesha Chelsea kusonga mbele licha ya kufungwa mabao 3-2 ugenini Rubin Kazan.
    Chelsea imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-4, baada ya awali kushinda 3-1 nyumbani.
    Mabao ya Chelsea jana yalifungwa na Fernando Torres dakika ya tano na Victor Moses dakika ya 55, wakati Kazan walipata mabao yao kupitia kwa Marcano dakika ya 51, Karadeniz dakika ya 62 na Natcho kwa penalti dakika ya 75.
    Kikosi cha Chelsea jana kilikuwa;Cech, Azpilicueta, Luiz, Terry, Ake, Ferreira, Benayoun/Oscar dk77, Ramires/Mikel dk 60, Lampard/Ivanovic dk90, Moses na Torres.
    Rubin Kazan: Ryzhikov, Kuzmin/Kaleshin dk45, Ansaldi, Cesar Navas, Marciano, Orbaiz/Dyadyun dk66, Natcho, Kasaev/Ryazantsev dk72, Karadeniz, Eremenko na Rondon.

    Masked hero: Fernando Torres is perhaps playing his best football since joining Chelsea
    Shujaa wa Mask: Fernando Torres akishangilia bao lake muhimu jana

    Newcastle ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Benfica ye Ureno, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2, baada ya awali kufungwa 3-1 ugenini. Bao la Newcastle lilifungwa na Papiss Cisse dakika ya 71 na Benfica lilifungwa na Salvio dakika ya 90.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TORRES AIPELEKA CHELSEA NUSU FAINALI ULAYA, SPURS NA NEWCASTLE NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top