• HABARI MPYA

    Thursday, April 11, 2013

    XAVI AVUNJA REKODI YA PASI ULAYA, AWAFUNIKA WOTE UNAOWAJUA


    HAKIKUWA kiwango bora kilichoonyeshwa na Barcelona, lakini kwa Xavi ulikuwa ni usiku mzuri wa kuukumbuka: akipatia kwa asilimia 100 katika pasi zake zote 96 alizopiga dhidi ya Paris St Germain jana.  
    Vigogo hao wa Catalan walitolewa jasho kupata nafasi ya kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa, walipokuwa nyuma kwa bao 1-0 ndani ya dakika ya 50 na hatimaye kufuzu tu kwa faida ya mabao ya ugenini, baada ya Pedro kusawazisha dakika ya 71. 
    Unblemished record: Xavi found an team-mate with every pass against Paris St Germain
    Rekodi: Xavi alimfikishia kila pasi kila mchezaji mwenzake aliyempelekea jana dhidi ya Paris St Germain
    Unblemished record: Xavi found an team-mate with every pass against Paris St Germain
    Wengi watasifia kuingia kwa Lionel Messi katikati ya kipindi cha pili kama siri ya mafanikio ya Barca jana, lakini alikuwa ni Xavi aliyecheza kwa ubora wa hali ya juu katika nafasi ya kiungo. 
    All smiles: Xavi savours success at the Nou Camp with team-mate Andres Iniesta
    Tabasamu: Xavi akifurahia kwenye Uwanja wa Nou Camp jana na mchezaji mwenzake Andres Iniesta
    Mspanyola huyo mwenye umri wa miaka, 33, alikaribia kufunga dakika ya kwanza tu baada ya shuti lake la mpira wa ashabu kudondokea nyuma ya nyavu na wengi uwanjani kudhani ni bao.  
    Alicheza dakika zote 90 katika mechi hiyo na alifanikiwa kumfikishia pasi kila mchezaji mwenzake aliyempelekea na kuwapiku wachezaji wengine wote kwa miaka 10.
    Kazi nzuri ya Xavi jana kwa asilimia 100 anawapiku Javier Zanetti dhidi ya Tottenham miaka mitatu iliyopita na nyota wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Eboue anayeshika nafasi ya tatu katika orodha. 
    Lakini wakati Mspanyola huyo anamudu kupiga pasi zake kwa asilimia 100, Zanetti na Eboue walipiga kwa usahihi pasi 72 na 54 katika mechi zao.   
    Inafahamika uwezo wa Cristiano Ronaldo unamfanya awepo katika orodha, lakini hamuachi mbali Nahodha wa Chelsea, John Terry aliyefanya kazi nzuri dhidi ya Werder Bremen kwenye michuano hiyo mwaka 2008.
    Catch him if you can: Xavi was instrumental in Barca's progress into the semi-finals of the Champions League
    Mkamate kama unaweza: Xavi alikuwa kila kitu Barca ikifuzu Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa jana
    Catch him if you can: Xavi was instrumental in Barca's progress into the semi-finals of the Champions League

    WAKALI WA PASI MURUWA LIGI YA MABINGWA TANGU MSIMU WA 2003/04 

    MECHIMWAKAMCHEZAJIIDADI YA PASI
    Barcelona v PSG2013Xavi96
    Inter vs Tottenham2010Javier Zanetti72
    FC Porto vs Arsenal2006Emmanuel Eboue54
    Barcelona vs Stuttgart2007Lilian Thuram50
    Real Madrid vs Man City2012Cristiano Ronaldo50
    Braga vs Galatasaray2012Paulo Vinicius 48
    Basel vs Barcelona2006Martin Caceres48
    Chelsea vs Werder Bremen2008John Terry47
    FC Porto vs Dynamo Kiev2006Rolando45
    Roma vs Real Madrid2004Ivan Helguera43
    Real Madrid vs Dinamo Zagreb2011Sergio Ramos43

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: XAVI AVUNJA REKODI YA PASI ULAYA, AWAFUNIKA WOTE UNAOWAJUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top