• HABARI MPYA

    Saturday, June 15, 2013

    LIONEL MESSI AMPIKU DIEGO MARADONA KWA MABAO ARGENTINA BAADA YA JANA KUPIGA MATATU PEKE YAKE KATIKA USHINDI WA 4-0

    IMEWEKWA JUNI 15, 2013 SAA 7:45 MCHANA
    MSHAMBULIAJI Lionel Messi amepiku rekodi ya Diego Maradona ya kufunga mabao katika timu ya taifa ya Argentina, baada ya jana usiku kufunga mabao matatu peke yake akiiwezesha nchi yake kuibwaga Guatemala 4-0 katika mchezo wa kirafiki.
    Nyota huyo wa Barcelona sasa analingana kwa mabao na Hernan Crespo, 35 kila mmoja lakini anazidiwa kwa mabao 21 na gwiji Gabriel Batistuta.
    Watu wamekuwa wakibishana sana juu ya uwezo wa Messi na Maradona kwamba nani zaidi kati yao, lakini nyota wa Barca akiwa na umri wa miaka 25 tu anaonyesha anaweza kustaafu akiwa mfungaji bora wa kihistoria kwa nchi yake.
    Nice work: Lionel Messi celebrates with Sergio Aguero (left) and (below) fires home his penalty kick
    kazi nzuri: Lionel Messi akishangilia na Sergio Aguero (kushoto) na chini akiifungia timu yake kwa Penalti
    Goal: Messi bangs it home from the spot
    Overtaken: Diego Maradona has 34 goals for Argentina and was their third top scorer of all-time
    Amepitwa: Diego Maradona ameifungia mabao 34 Argentina na alikuwa anashika nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji wa kihistoria
    Diego
    Messi
    Utamchagua nani? Ubishani kwamba nani zaidi kati ya Messi (kulia) na Maradona (kushoto)

    Alirejea kwenye kikosi cha kwanza baada ya kuwekwa benchi katika mechi mbili zilizopita kutokana na kuwa majeruhi.
    Alifunga bao la kwanza kwa shuti la mbali, kabla ya kumtengenezea nafasi ya kufunga bao la pili Augusto Fernandez kisha akafunga kwa penalti kufikisha idadi ya mabao ya Maradona kabla ya mapema kipindi cha pili kufunga bao la kumpiku gwiji huyo, akiunganisha pasi ya Ezequiel Lavezzi.
    Batigol: Gabriel Batistuta is Argentina's all-time top scorer with Hernan Crespo (below) now level with Messi
    Batigol: Gabriel Batistuta ndiye mfungaji bora wa kihistoria wa Argentina akiwa mbele ya Hernan Crespo (chini) na sasa na Messi pia
    Hernan
    Lakini kocha wa zamani wa ufiti wa Argentina, Fernando Signorini ameonya kwamba Messi anaweza akawa hayuko vizuri wakati wa Fainali za Kombe la Dunia mwakani kutokana na kutumika sana.
    "Kabla, Miaka ya 60 na 70, wachezaji walikuwa wanacheza mechi 80 hadi 90 kwa mwaka, lakini (Messi), ni nambari moja duniani, anacheza mechi zaidi ya 120 kama ukihesabu mechi zake za Barcelona na timu ya taifa,"alisema na kunukuliwa na Marca.
    "Messi amecheza miaka mitatu bila kuumia, lakini miezi miwili na nusu iliyopita aliumia misuli kabla ya Nusu Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich nchini Ujerumani, na akawekwa benchi katika mchezo wa marudiano. Kisha akaumia tena,"alisema.
    Worries: Messi might not be 100 per cent at the World Cup because of the amount of matches he plays
    Wasiwasi: Messi anaweza asiwe vizuri kwa asilimia 100 wakati wa Kombe la Dunia kwa sababu ya kutumika sana

    VIDEO: Angalia Messi alivyompiku Maradona
     

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: LIONEL MESSI AMPIKU DIEGO MARADONA KWA MABAO ARGENTINA BAADA YA JANA KUPIGA MATATU PEKE YAKE KATIKA USHINDI WA 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top