• HABARI MPYA

    Sunday, June 30, 2013

    MASWAHIBA WA PELE, AZAM AKADEMI WAENDA KUTETEA TAJI ARUSHA WAKIWA KAMILI

    Maswahiba wa Pele; Azam Akademi wakiwa na Pele alipowatembelea Chamazi mwaka jana
    Na Prince Akbar, IMEWEKWA JUNI 30, 2013 SAA 2:25 ASUBUHI
    MABINGWA watetezi wa Kombe la Rollingstone, michuano ya kila mwaka mjini Arusha, Azam Akademi wanatarajiwa kuondoka wiki ijayo kwenda mjini humo tayari kutetea taji lao.
    Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, Akademi wamekuwa kwenye mazoezi makali chini ya makocha wao, Vivek Nagul, Iddi Cheche na Philipo Alando kujiandaa na michuano hiyo.
    Amesema maandalizi ya vijana yamekuwa ya muda mrefu na sasa wako fiti kwenda kuendeleza utemi wao katika michuano hiyo maarufu zaidi ya vijana nchini kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
    “Kama unavyojua hii ni akademi, vijana muda wote wanakuwa chuoni wakipata mafunzo mbalimbali, wanahudumiwa vizuri na wanafanya mazoezi kila siku asubuhi na jioni kwenye Uwanja wetu wa Azam Complex, Chamazi. Hivyo nakuhakikishia wako fiti na tayari kabisa,”alisema.
    Akademi ya Azam inatarajiwa kuwa moja ya vyanzo vikuu vya nyota wa soka nchini baadaye na hata Mwanasoka Bora wa zamani wa Afrika, Abedi Pele alipotembelea akademi hiyo mwaka jana aliitabiria makubwa.
    Pele, aliyeongozana na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chilla Tenga Chamazi, alisema akademi hiyo ni bora kuliko nyingi za Ulaya na akasema wakati utafika itakuwa inapeleka wachezaji Ulaya. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MASWAHIBA WA PELE, AZAM AKADEMI WAENDA KUTETEA TAJI ARUSHA WAKIWA KAMILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top