• HABARI MPYA

    Sunday, June 30, 2013

    PELLEGRINI SASA ATAKA KUMSAJILI FRED WA BRAZIL NA CARDOZO WA BENFICA KUTENGENEZA PACHA JIPYA HATARI LA USHAMBULIAJI MAN CITY

    IMEWEKWA JUNI 30, 2013 SAA 1:00 ASUBUHI
    KOCHA wa Manchester City, Manuel Pellegrini amehamishia mawindo yake kwa washambuliaji Mbrazil, Fred na Oscar Cardozo wa Benfica, baada ya kuamua kuachana na Edinson Cavani aliyekuwa anatakiwa na kocha aliyemtangulia, Roberto Mancini aliyetimuliwa.
    Pellegrini, ambaye amepewa kauli ya mwisho kuhusu usajili katika klabu hiyo licha ya kuwepo kwa Mkurugenzi wa Soka, Txiki Begiristain, hataki City ibomoe benki kwa ajili ya Cavani, baada ya klabu yake, Napoli kukataa ofa iliyotolewa ya Pauni Milioni 54. 
    Premier player: Brazil's Fred (left) is a target for Manchester City
    Mchezaji Mkuu: Fred wa Brazil (kushoto) anatakiwa Manchester City
    City bound: Oscar Cardozo could be a ready replacement for Carlos Tevez
    Anayewatoa udenda City: Oscar Cardozo anaweza kuchukua nafasi ya Carlos Tevez
     
    Mshambuliaji wa Fluminense, Fred, ambaye ataiongoza nchi yake leo katika Fainali ya Kombe la Mabara dhidi ya Hispania, kwa sasa anatabirwa kwenda kuziba pengo la Carlos Tevez, aliyejiunga na Juventus wiki iliyopita. 
    Fred, mwenye umri wa miaka 29, alifunga wakati Brazil inatoa sare ya 2-2 na England mapema mwezi huu na akafunga mabao mawili dhidi ya Italia katika michuano hii ya kupashia misuli moto Kombe la Dunia inayofikia tamati leo. 
    Cardozo, mshambuliaji wa Montenegro, Stevan Jovetic na Stephan El Shaarawy, wa AC Milan, pia wametajwa kama wawania kurithi mikoba ya Tevez huku Pellegrini akitarajia kutengeneza alama yake katika klabu hiyo kabla hajaanza mazoezi ya kujiandaaa na msimu mpya. 
    Kwa muda mrefu, Mancini alimfanya mshambuliaji wa Uruguay, Cavani chaguo la kwanza katika wachezaji anaowataka, lakini akafukuzwa City siku kadhaa baada ya kufungwa kwenye Fainali ya Kombe la FA na Wigan mwezi uliopita.
    Pellegrini, ambaye aliiongoza Malaga kutinga Robo Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, anataka kuongeza mshambuliaji na na sentahafu, baada ya kukamilika kwa usajili wa winga wa Hispania, Jesus Navas na kiungo wa Brazil, Fernandinho. 
    City inataka kukata Pauni Milioni 20 kumnunua beki wa kati wa Real Madrid, Pepe, ambaye atatengeneza ushirikiano mpya na Vincent Kompany.
    Mpango wao wa sasa kutaka kumsajili Pepe ni pigo kubwa kwa beki wa sasa wa City, Joleon Lescott, ambaye anatarajia kuwa na mazungumzo na klabu hivi karibuni juu ya mustakabali wake.
    Lescott, mwenye umri wa miaka 31, anataka uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza, ili kulinda nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa ya England, kuelekea Fainali za Kombe la Dunia mwakani, Brazil.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: PELLEGRINI SASA ATAKA KUMSAJILI FRED WA BRAZIL NA CARDOZO WA BENFICA KUTENGENEZA PACHA JIPYA HATARI LA USHAMBULIAJI MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top