• HABARI MPYA

    Saturday, June 29, 2013

    ROONEY HABAKI MAN UNITED, MOYES SASA KAZI ANAYO...KIJANA MGUU NJIANI KUELEKEA DARAJANI

    IMEWEKWA JUNI 29, 2013 SAA 1:13 ASUBUHI
    KOCHA David Moyes atakabiliwa na mwanzo mgumu atakapoanza tu kazi Manchester United, baada ya kubainika Wayne Rooney bado ana msimamo wa kuondoka Old Trafford.
    Kocha huyo wa zamani wa Everton anayeanza kazi rasmi Jumatatu Manchester United, alitumai kumshawishi Rooney kusahau tofauti zake na kocha aliyestaafu Sir Alex Ferguson na kuelekeza nguvu zake katika kuiwezesha klabu kutetea ubingwa wa Ligi Kuu.
    Mind elsewhere: Wayne Rooney was at Glastonbury on Friday as he contemplates his future
    Popote poa: Wayne Rooney alikuwa Glastonbury Ijumaa katika sehemu ya likizo yake
    Mind elsewhere: Wayne Rooney was at Glastonbury on Friday as he contemplates his future
    Mind elsewhere: Wayne Rooney was at Glastonbury on Friday as he contemplates his future
    Lakini, katika hatua ambayo itamuweka mkao wa kula kocha mpya wa Chelsea, Jose Mourinho, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hayuko katika dalili za kughairi juu ya mpango wake na anatarajiwa kumuambia Moyes bado anataka kuondoka.
    BIN ZUBEIRY inafahamu kupitia Sportsmail kwamba United imeanza kupanga maswali ya kumuuliza mshambuliaji huyo wa England, aliyewagharimu Pauni Milioni 27 walipomsajili kutoka Everton mwaka 2004.
    Job on his hands: David Moyes looks set to miss out on working with Rooney for a second time
    Kazi ipo mikononi mwake: David Moyes anatarajiwa kupoteza fursa ya kufanya kazi na Rooney kwa mara ya pili
    Job on his hands: David Moyes looks set to miss out on working with Rooney for a second time
    Ikiwa Moyes atafeli katika mazungumzo yake na Rooney, United italazimika kumuuza kwa angalau Pauni Milioni 25.
    Chelsea inaonekana kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya Arsenal kumpata mpachika mabao huyo, na hiyo inatokana na kambi ya Rooney kwamba haijaamua akacheze nje.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ROONEY HABAKI MAN UNITED, MOYES SASA KAZI ANAYO...KIJANA MGUU NJIANI KUELEKEA DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top