• HABARI MPYA

    Wednesday, July 17, 2013

    ARSENAL YAENDELEZA MAUWAJI, YAWAFUMUA 7-1 WAVIETNAM LEO

    IMEWEKWA JULAI 17, 2013 SAA 5:00 USIKU
    ARSENAL imeendeleza wimbi la ushindi mnono katika mechi za kujiandaa na msimu, baada ya leo kuifumua mabao 7-1 Vietnam XI kwenye Uwanja wa My Dinh mjini Hanoi.
    Ushindi huo umemoa majibu kadhaa kocha Arsene Wenger, kwanza kama atashindwa kusajili mshambuliaji wa kiwango cha dunia kabla ya mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu England dhidi ya Aston Villa, Olivier Giroud atatosha kwenye kampeni ya ushindi baada ya leo kufunga mabao matatu peke yake.
    Pili, anaweza kumtumia Bacary Sagna katika beki ya kati itakapotokea dharula kama atakwama kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams baada ya beki huyo kulia wa Arsenal kucheza namba nzuri leo.
    Na tatu, inayoweza kuwa muhimu kuliko zote, Jack Wilshere na kama yuko fiti kabisa kuanza msimu, baada ya kucheza mechi yake ya kwanza leo tangu afanyiwe upasuaji wa kifundo cha mguu Mei.
    Thanks! The Arsenal players carry a 'Thank You' banner and wave to fans after defeating Vietnam
    Shukrani! Wachezaji wa Arsenal wakiwa wamebeba bango la 'Asanteni' kwa ajili ya mashabiki baada ya kuwafunga Vietnam
    Challenge: Arsenal's Bacary Sagna tackles Vietnam's Nguyen Anh Duc
    Shughuli: Beki wa Arsenal, Bacary Sagna akiupitia mpira miguuni mwa Nguyen Anh Duc wa Vietnam

    Mbali na mabao matatu ya Giroud, mabao mengine ya Arsenal leo yamefungwa na Alex Oxlade-Chamberlain, Chuba Akpom mawili na Ignasi Miquel ambao wote walifunga pia kwenye ushindi wa 7-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Dream Team ya Indonesia.
    Kikosi cha Arsenal leo kilikuwa; Szczesny/Martinez dk71, Sagna/Aneke dk71, Jenkinson/Olsson dk71, Koscielny/Mertesacker dk46, Gibbs/Miquel dk46, Arteta (Nahodha)/Ramsey dk46, Rosicky/Zelalem dk46, Oxlade-Chamberlain/Wilshere dk66, Gnabry/Walcott dk46, Podolski/Miyaichi dk46 na Giroud/Akpom dk46
    Watching it fly in: Olivier Giroud scores one of his goals against Vietnam
    Olivier Giroud akifunga moja ya mabao yake leo
    Put it there: Chuba Akpom celebrates his goal with his teammate Alex Oxlade-Chamberlain
    Chuba Akpom akishangilia bao lake na mchezaji mwenzake, Alex Oxlade-Chamberlain
    Break through: Giroud strides past his opponent during a very straightforward victory for Arsenal
    Giroud akifanya safari
    Chuba Akpom
    Chuba Akpom
    Chuba Akpom akishangilia bao lake leo
    Serge surge: Serge Gnabry takes on the Vietnam defence
    Serge Gnabry akipasua ngome ya Vietnam
    Speedster: Alex Oxlade-Chamberlain was also on target during the 7-1 win
    Alex Oxlade-Chamberlain pia alifunga leo
    Battle: Vietnam's Pham Thanh Luong vies for the ball with Arsenal's Bacary Sagna

    RATIBA YA MECHI ZA ARSENAL KUJIANDAA NA MSIMU

    Julai 14 na Indonesia XI walishinda 7-0
    Julai 17 na Vietnam wameshinda 7-1
    Julai 22 na Nagoya Grampus (Uwanja wa Toyota, Japan) Saa 5.30 asubuhi
    Julai 26 na Urawa Red Diamonds (Uwanja wa Saitama, Japan - Kombe la Saitama City) Saa 5.30 asubuhi
    Agosti 3 na Napoli (Kombe la Emirates) Saa 10.20 jioni
    Agosti 4 na Galatasaray (Kombe la Emirates) Saa 10.20 jioni
    Agosti 10 na Manchester City (Uwanja wa Olimpiki, Helsinki) Saa 9 jioni
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ARSENAL YAENDELEZA MAUWAJI, YAWAFUMUA 7-1 WAVIETNAM LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top