• HABARI MPYA

    Sunday, July 07, 2013

    MAN CITY KARIBU KABISA KUMSAJILI MFUNGAJI BORA LA LIGA ALIYEWAFUATIA MESSI NA RONALDO

    IMEWEKWA JULAI 7, 2013 SAA 11:45 ALFAJIRI
    MSHAMBULIAJI Alvaro Negredo anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 20 kutua Manchester City wiki hii.
    Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 wa Sevilla, ambaye alikaribia kujiunga na Atletico Madrid, lakini nia ya kuchezea timu inayofundishwa na Manuel Pellegrini, City imeelezwa kumfanya abadili njia na sasa anakuja KLigi Kuu ya England.
    Perfect fit: Manuel Pellegrini feels Alvaro Negredo will suit Manchester City
    Fiti kabisa: Manuel Pellegrini anafikiri Alvaro Negredo atafaa Manchester City
    Right move: Manuel Pellegrini has convinced Alvaro Negredo to join City
    Hatua sahihi: Manuel Pellegrini amemshawishi Alvaro Negredo kujiunga na City
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Hispania, alimaliza wa nne katika ufungaji bora wa La Liga msimu uliopita kwa mabao yake 25 katika ligi hiyo, alitaka kusajiliwa na Pellegrini wakati alipokuwa Malaga, lakini dili hilo halikufanikiwa.
    City inataka kuboresha safu yake ya ushambuliaji baada ya kuwauza Mario Balotelli kwenda AC Milan Januari mwaka huu na Carlos Tevez kwenda Juventus mwezi uliopita.
    Klabu hiyo ilikuwa inamtaka mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani, ambaye yuko mbioni kutua Paris St Germain kwa Pauni Milioni 50, dau ambalo limemkatisha tamaa Pellegrini na sasa anaelekeza nguvu zake kwa Negredo, aliyeanzia soka katika kikosi cha wachezaji wa akiba wa Real Madrid, akiamini atafanya vizuri City.
    That's rich: City look set to miss out on Uruguay's Edinson Cavani
    Tajiri: City inatarajiwa kumkosa nyota wa Uruguay, Edinson Cavani
    Transfer trail: Atletico Madrid could move for City striker Edin Dzeko if they miss out on Negredo
    Ataondoka?: Atletico Madrid inaweza kumtaka mshambuliaji Edin Dzeko ikiwa watamkosa Negredo
    Atletico Madrid inaweza kuhamia kwa Edin Dzeko ikiwa watampoteza kwa City, Negredo, mchezaji wa zamani wa mchezaji mpya aliyesajiliwa majira haya joto,  Jesus Navas.
    Mshambuliaji wa kimataifa wa Bosnia, Dzeko amekuwa pia akihuishwa na mpango wa kuhamia Napoli kama mbadala wa Edinson Cavani anayeweza kutua PSG kwa Pauni Milioni 53.However, Rafa Benitez is considering other targets.

    Pellegrini atafurahi Dzeko akibaki City, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anataka kucheza na kuuzwa kwake, kutatoa nafasi kwa wengine kama Negredo na beki wa Real Madrid, Pepe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MAN CITY KARIBU KABISA KUMSAJILI MFUNGAJI BORA LA LIGA ALIYEWAFUATIA MESSI NA RONALDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top