• HABARI MPYA

    Wednesday, April 16, 2014

    ARSENAL YAIFUMUA WEST HAM 3-1 NA KUFUFUA MATUMAINI YA KUICHEZA LIGI YA MABINGWA

    ARSENAL imeichapa mabao 3-1 West Ham Unitede Uwanja wa Emirates jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya England na kufufua matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
    Mabao ya Gunners jana yamefungwa na Lukas Podolski mawili dakika za 44 na 78 na Olivier Giroud dakika ya 54. Ushindi huo unaifanya Arsenal itimize pointi 67 baada ya kucheza mechi 34 na kuendelea kukamata nafasi ya nne.
    Liverpool ipo kileleni kwa pointi zake 77 za mechi 34, Chelsea ya pili pointi 75 za mechi 34, wakati Manchester City ni ya tatu kwaq pointi zake 70 za mechi 32. 
    Kazi nzuri: Lukas Podolski ameifungia mabao mawili Arsenal ikiichapa 3-1 West Ham janaBack of the net: Arsenal striker Olivier Giroud powers home the Gunners second
    Kitu nyavuni: Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud amefunga moja jana
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAIFUMUA WEST HAM 3-1 NA KUFUFUA MATUMAINI YA KUICHEZA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top