• HABARI MPYA

    Tuesday, April 15, 2014

    BARCELONA WATWAA TAJI LA LIGI YA MABINGWA ULAYA KWA VIJANA, KINDA WAKE AFUNGA KUTOKA KATIKATI YA UWANJA

    KINDA Munir El Haddadi jana alifunga bao tamu kutoka katikati ya Uwanja Barcelona ikitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa vijana chini ya umri wa miaka 19 kwa kuifunga Benfica mabao 3-0 mjini Nyon, Usiwsi.
    Munir alifunga mabao mawili jumla jana dakika za 33 na 87, wakati bao lingine lilifungwa na Rodrigo Tarin dakika ya tisa.
    Timu ya kwanza ya Barca ipo katika wakati mgumu hivi sasa ikiwa imetolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na wapinzani wao Hispania, Atletico Madrid  na ikafungwa 1-0 na Granada Jumamosi katika La Liga.
    Na baada ya kufungiwa kusajili hadi mwaka 2015 na FIFA, adhabu ambayo wameikatia rufaa, Wakatalunya hao wanaweza kupandisha viranga vyao vya akademi.

    Wafalme: Nahodha wa Barca, Roger Riera akiwa ameshika taji la Ligi ya Mabingwa kwa vijana jana baada ya ushindi
    The future: Munir El Haddadi celebrates after sealing Barca's 3-0 win against Benfica
    Nyota wa baadaye: Munir El Haddadi akisherehekea ushindi wa Barca wa 3-0 jana
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCELONA WATWAA TAJI LA LIGI YA MABINGWA ULAYA KWA VIJANA, KINDA WAKE AFUNGA KUTOKA KATIKATI YA UWANJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top