• HABARI MPYA

    Wednesday, April 16, 2014

    MAN CITY YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 ETIHAD NA SUNDERLAND


    MATUMAINI ya Manchester City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England, yameanza kufifia baada ya usiku huu kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Sunderland Uwanja wa Etihad. 
    Fernandinho alitangulia kuifungia Manchester City dakika ya pili akimalizia pasi ya Sergio Aguero, lakini kinda wa umri wa miaka 21 wa England, Connor Wickham akaisawazishia Sunderland dakika ya 73 kwa pasi ya Mtaliano Emanuele Giaccherini. 
    Wickham akaifungia bao la pili Sunderland dakika ya 83 kwa pasi ya Giaccherini tena, lakini Mfaransa Samir Nasri akainusuru City kuzama kwa kuisawazishia dakika ya 88 kwa pasi ya Jovetic.
    Huyu hapa; Kinda aliyeifungia Sunderland mabao mawili leo,Wickham akishangilia
    Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja City na kufikisha 71 baada ya kucheza mechi 33, ikiendelea kubaki nafasi ya tatu nyuma ya Chelsea yenye pointi 75 za mechi 34 na Liverpool pointi 77 za mechi 34 pia.
    Katika mchezo mwingine, Crystal Palace imeichapa Everton mabao 3-2 Uwanja wa Goodison Park. Mabao ya washindi yamefungwa na Puncheon dakika ya 23, Dann dakika ya 49 na Jerome dakika ya 73, wakati mabao ya wenyeji yamefungwa na Naismith dakika ya 61 na Mirallas dakika ya 86.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 ETIHAD NA SUNDERLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top