• HABARI MPYA

    Tuesday, April 15, 2014

    MKWASA: SIMBA HAWATATUFUNGA KIZEMBE TENA

    Na Renatus Mahima, Arusha
    KOCHA msaidizi wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema timu yao kamwe haitafungwa kizembe tena na watani wao wa jadi Simba ikama ilivyokuwa katika mechi yao iliyopita.
    Yanga ilifungwa kizembe 3-1 dhidi ya Simba katika mechi ya 'Nani Mtani Jembe' kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Desemba 21, mwaka jana, mechi ya 'ndondo' iliyowafukuzisha kazi makocha Ernie Brandts raia wa Uholanzi na mzawa Felix Minziro.
    Kikosi cha Yanga SC kilichocheza na JKT Ruvu juzi

    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jijini hapa mara tu baada ya mechi yao ya raundi ya 25 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara walioshinda 2-1 dhidi ya Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa leo mchana, Mkwasa amesema hawako tayari kuona tena timu yao inafungwa magoli ya kizembe na Simba katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Simba msimu huu kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi.
    "Tumekosa ubingwa lakini hatuko tayari kufungwa kizembe na Simba katika mechi ya mwisho," alisema Mkwasa.
    Katika hatua nyingine, kocha wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema licha ya kukifunga magoli 2-1, kikosi cha Oljoro JKT kilichoshuka daraja ni kigumu kufungika.
    "Ilikuwa mechi ngumu hasa kipindi cha pili, tumecheza na timu ngumu na ninashangaa kuambiwa inashuka daraja," amesema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKWASA: SIMBA HAWATATUFUNGA KIZEMBE TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top