• HABARI MPYA

    Tuesday, April 15, 2014

    WELBECK, ASHLEY YOUNG NA CLEVERLEY WAPIGWA FAINI MAN UNITED BAADA YA KUJIRUSHA NA DEMU USIKU KUCHA

    WACHEZAJI Danny Welbeck, Tom Cleverley na Ashley Young wamepigwa faini na kupewa onyo kali baada ya kujirusha usiku kucha wakiwa na demu saa kadhaa tu baada ya Manchester United kutolewa katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Wanasoka hao wa kimataifa wa England walipigwa picha jijini Manchester usiku wa Ijumaa iliyopita hadi asubuhibaada ya kurejea kutoka Munich Alhamisi ambako Jumatano walitolewa na Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa.
    Kocha David Moyes aliwaita watatu hao kuzungumza nao jana makao makuu ya United, Carrington kabla ya kuwataka wafanye mazoezi ya ziada tofauti na wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo. 
    Wachezaji wote watatu wamepigwa faini, ingawa haiko wazi kama wamekatwa mishahara ya wiki mbili au tatu.
    Kujirusha kumewaponza: Welbeck kushoto akizungumza na demu waliyekuwa wakicheza naye na kulia ni Cleverley

    Moyes, ambaye atamenyana na klabu yake ya zamani Everton Uwanja wa Goodison Park Jumapili, ana mpango wa kutumia Pauni Milioni 150 kusajili mwishoni mwa msimu ili kukijenga upya kikosi chake.
    Habari njema kwa Moyes, ni kupata nafuu kwa mshambuliaji Robin van Persie kutoka maumivu yake ya goti.
    Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi ameweka ciedo kwenye Facebook inayomuonyesha akifanya mazoezi peke yake gym.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WELBECK, ASHLEY YOUNG NA CLEVERLEY WAPIGWA FAINI MAN UNITED BAADA YA KUJIRUSHA NA DEMU USIKU KUCHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top