• HABARI MPYA

    Thursday, August 21, 2014

    SIMBA NA YANGA OKTOBA 12 NA FEBAURI 8, MECHI ZAO NA AZAM FC…RATIBA KAMILI LIGI NZIMA HII HAPA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    WATANI wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba SC na Yanga watakutana Oktoba 12, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mzunguko wa kwanza, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Ladha ya Ligi Kuu ni mechi baina ya miamba hiyo miwili nchini- na kidogo mechi zinazozihusisha timu hizo na mabingwa watetezi, Azam FC, nazo pia huwa za kukata na shoka.
    Msimu uliopita, mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya 3-3, Simba wakitoka nyuma kwa 3-0 hadi mapumziko na marudiano, Yanga walisawazisha dakika za lala salama kupata sare ya 1-1.
    Kocha Patrick Phiri wa Simba SC atakutana na watani Yanga SC, Oktoba 12 mwaka huu Uwanja wa Taifa
    Lakini Simba SC ilijichukulia ubabe wa jumla wa msimu dhidi ya watani wao, baada ya kuwafunga Yanga SC 3-1 katika mchezo wa Nani Mtani Jembe Desemba mwaka jana Uwanja wa Taifa.
    Mzunguko wa pili, timu hizo zitakutana Februari 8, mwakani, mchezo wa kwanza Yanga mwenyeji, wa pili Simba mwenyeji.
    Azam FC na Simba zitakutana Januari 1, mwaka 2015 wakati marudiano yatakuwa ni Aprili 12, mwaka huo.
    Yanga itamenyana na Azam FC Novemba 9, mwaka huu wakati mchezo wa marudiano utapangiwa siku. Ikumbukwe Septemba 13, Yanga na Azam FC zitafungua pazia la Ligi Kuu kwa mchezo wa Ngao ya Jamii Uwanja wa Taifa.
    INGIA HAPA KUANGALIA RATIBA KAMILI: http://habarimoto.blogspot.com/2014/08/ratiba-nzima-ligi-kuu-bara-20142015.html

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA YANGA OKTOBA 12 NA FEBAURI 8, MECHI ZAO NA AZAM FC…RATIBA KAMILI LIGI NZIMA HII HAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top