• HABARI MPYA

    Wednesday, September 17, 2014

    BALE, RONALDO, RODRIGUEZ WOTE WAFUNGA REAL MADRID IKIPIGA MTU MKONO

    MABINGWA wa Ulaya, Real Madrid wameanza kwa kishindo kutetea taji, baada ya usiku huu kuifumua mabao 5-1 Basle Uwanja wa Bernabeu.
    Marek Suchy alijifunga dakika ya 14 kuipa Real bao la kuongoza kabla ya Gareth Bale kufunga la pili akimalizia pasi ya Luka Modric dakika ya 30.
    Bale akamtilia krosi maridadi Cristiano Ronaldo kuifungia Real bao la tatu dakika ya 31 kabla ya James Rodriguez kufunga la nne dakika ya 36 na Derlis Gonzalez kuifungia Basle bao la kufutia machozi dakika ya 37. Karim Benzema alihitimisha shangwe za mabao za Real Madrid kwa bao la tano dakika ya 79.
    Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Pepe, Sergio Ramos, Marcelo, Nacho, Kroos, Rodriguez, Bale, Modric, Ronaldo na Benzema. 
    Basle: Vaclik, Samuel, Schar, Suchy, Safari, Zuffi, Frei, El-Nenny, Xhaka, Streller na Gonzalez.
    Gareth Bale akipongezana na Ronaldo baada ya kufunga katika ushindi wa 5-1
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BALE, RONALDO, RODRIGUEZ WOTE WAFUNGA REAL MADRID IKIPIGA MTU MKONO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top