• HABARI MPYA

    Monday, September 01, 2014

    DANIEL AGGER AONDOKA LIVERPOOL, AREJEA BRONDBY

    BEKI Daniel Agger amerejea klabu yake ya zamani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006 baada ya Mdenmark huyokukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 3 kujiunga na Brondby. 
    Mlinzi huyo wa kati mwenye umri wa miaka anakwenda klabu hiyo ya Denmark kwa Pauni Milioni 3 baada ya kupiga kazi Anfield kwa miaka nane.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Denmark amecheza jumla ya mechi 232 klabu hiyo ya Merseyside, lakini ametwaa taji moja tu, Kombe la Ligi mwaka 2012, maarufu kama Carling Cup Uwanja wa Wembley.

    Amerudi nyumbani: Daniel Agger akiwa na jezi ya Brondby  baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Liverpool
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DANIEL AGGER AONDOKA LIVERPOOL, AREJEA BRONDBY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top