• HABARI MPYA

    Monday, September 01, 2014

    FALCAO ATUA MAN UNITED KWA MKOPO WA MWAKA MMOJA

    KLABU ya Manchester United imeshinda mbio za kuwania saini ya mshambuliaji Radamel Falcao kutoka Monaco kwa mkopo wa mwaka mmoja.
    Mpachika mabao huyo ataigharimu klabu hiyo ya Old Trafford Pauni Milioni 12 kwenda kuungana na Angel di Maria, Daley Blind, Luke Shaw, Ander Herrera na Marcos Rojo katika orodha ya wachezaji wapya kwenye kikosi cha Louis van Gaal.
    Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia mwenye umri wa miaka 28 tayari ameafiki kulipwa mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki na anatarajiwa kutua Manchester wakati wowote kwa ndege binafasi kukamilisha taratibu.
    Kimeeleweka: Manchester United imemnasa Radamel Falcao kwa mkopo kutoka Monaco

    REKODI YA FALCAO...

    River Plate (2005-2009): Mechi 105 mabao 45
    Porto (2009-2012): Mechi 87 mabao 72
    Atletico Madrid (2011-2013): Mechi 91 mabao 70
    Monaco (2013-2014): Mechi 22 mabao 13
    Colombia: Mechi 51 mabao 20
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FALCAO ATUA MAN UNITED KWA MKOPO WA MWAKA MMOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top