• HABARI MPYA

    Thursday, September 18, 2014

    GERVINHO AITAKATISHA AS ROMA LIGI YA MABINGWA

    MSHAMBULIAJI Gervinho na Nahodha mkongwe wa umri wa miaka 37, Francesco Totti wamefanya kazi nzuri usiku huu AS Roma ikiifumua CSKA Moscow mabao 5-1 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Olimpico.
    Gervinho amefunga mabao mawili na kuseti lingine moja lililofungwa na mchezaji mpya, Juan Iturbe wakati mabao mengine yamefungwa na Maicon na Totti, wakati bao pekee la CSKA limefungwa na Ahmed Musa. Bahati mbaya kwao Roma, Iturbe aliumia kipindi cha kwanza na kutoka.
    Katika michezo mingine, Athletic Bilbao imelazimishwa safe ya 0-0 na Shakhtar Donetsk wakati Porto iliichapa 6-0 BATE jana.
    Gervinho ameng'ara Roma ikiua 5-1 Ligi ya Mabingwa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GERVINHO AITAKATISHA AS ROMA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top