• HABARI MPYA

    Friday, September 19, 2014

    HUJUMA STARS, TFF KUUNDA JOPO LA KUCHUNGUZA, VIGOGO KUITWA KUHOJIWA

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa zilizoandikwa kwenye baadhi ya Vyombo vya Habari zikielezea tuhuma za hujuma kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) katika mechi za kufuzu mashindano ya AFCON.
    TFF pamoja na kutokuwa na uthibitisho wa tuhuma hizi nzito haliwezi kuzikalia kimya. TFF itateua jopo la kuchunguza tuhuma hizi.
    Wanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania (Members of TFF Family) watakaohitajika kuhojiwa na jopo hilo kwa mujibu wa Ibara ya 37 ya Kanuni za Maadili za TFF watalazimika kutoa ushirikiano. Atakayeshindwa kutoa ushirikiano atachukuliwa hatua za kimaadili.
    Taifa Stars ilitolewa na Msumbiji katika hatua za awali AFCON

    Pia wadau wa mpira wa miguu ambao sio wanafamilia wa TFF, watakaoitwa na jopo hili wanaombwa watoe ushirikiano kwa nia ya kujenga mpira wetu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HUJUMA STARS, TFF KUUNDA JOPO LA KUCHUNGUZA, VIGOGO KUITWA KUHOJIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top