• HABARI MPYA

    Sunday, September 14, 2014

    MAN UNITED YAANZA LIGI, YAITANDIKA QPR 4-0 DI MARIA AKIFUNGUA BIASHARA

    MANCHESTER United ya Louis Van Gaal imeanza ligi. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia Mashetani hao Wekundu kuifumua mabao 4-0 QPR katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford. 
    Winga Muargentina, Angel di Maria ndiye aliyefungua pati la mabao United leo baada ya kufunga bao la kwanza kwa mpira wa adhabu dakika ya 24.
    Angela Di Maria akishangilia na Wayne Rooney baada ya kufunga bao la kwanza

    Ander Herrera akaifungia Manchester United bao la pili dakika ya 35 kabla ya Wayne Rooney kufunga la tatu dakika ya 44 na Juan Mata akapiga la nne dakika ya 58. 
    Radamel Falcao alianzia benchi, akaingia dakika ya 67 kuchukua nafasi ya Juan Mata.
    Kikosi cha Man Utd kilikuwa: De Gea, Rafael/Valencia dk67, Evans, Rojo, Blackett, Blind, Herrera, Mata, Di Maria/Januzaj dk82, Rooney, Van Persie
    QPR: Green, Isla, Ferdinand, Caulker, Hill/Traore dk46, Sandro/Henry dk74, Kranjcar, Fer, Phillips, Austin/Vagas dk59, Hoilett.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YAANZA LIGI, YAITANDIKA QPR 4-0 DI MARIA AKIFUNGUA BIASHARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top