• HABARI MPYA

    Tuesday, September 30, 2014

    UKUTA WA YANGA SC WAENDELEA KUTESA STARS, NOOIJ AITA 26 WA KUIVAA BENIN

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij ameteua wachezaji 26 kwa ajili mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
    Kocha Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), safu ya ulinzi itaendelea kutegemea mabeki wa Yanga SC kwa mujibu wa kikosi alichoteua ambacho kitaingia kambini Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
    Kikosi cha Taifa Stars kitaendelea kutegemea safu ya ulinzi ya Yanga SC

    Wachezaji walioitwa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam).
    Mabeki ni Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).
    Viungo ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna Chanongo (Simba).
    Washambuliaji ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UKUTA WA YANGA SC WAENDELEA KUTESA STARS, NOOIJ AITA 26 WA KUIVAA BENIN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top