• HABARI MPYA

    Monday, October 20, 2014

    MANNY PACQUIAO AWEKA NDONDI KANDO NA KUPIGA MPIRA WA KIKAPU, AFANYE MAMBO WE ACHA TU!

    BONDIA Manny Pacquiao aliweka kando kidogo masumbwi na kuingia kwenye kizimba cha mpira wa kikapu wikiendi hii, alipocheza mechi yake ya kwanza Jumapili, mwezi mmoja kabla ya kutetea taji lake WBO uzito wa Welter.
    Pacquiao alianza katika mchezo wa jana akiichezea timu mpya iliyoundwa, KIA Sorento katika Ligi ya Chama cha Kikapu Ufilipino.
    Mkongwe huyo mwenye umri wa mkaka 35 alicheza kwa dakika saba tu na kubinjuka mara mbili, akiisaidia timu yake kushinda kwa vikapu 80-66 dhidi ya Blackwater Elite Uwanja wa Philippine Arena.
    Bondia wa Filipino, Manny Pacquiao akitupia mpira kwenye mchezo wake wa kwanza wa kikapu Jumapili
    Pacquiao attempts to dribble past two opposition players during his first game for KIA Sorento
    Pacquiao akipasua katikati ya wachezaji wa KIA Sorento
    The 35-year-old is more accustomed to fighting in the ring than shooting hoops on the court
    Huu ndiyo mchezo wake bondia huyo, lakini sasa ametambulisha kipaji kingine mbali ya pia kuwa mwanasiasa
    Nyota huyo wa ndondi amejiunga na timu hiyo mpya ya kikapu kama kocha mchezaji, akicheza mechi ya kujiandaa na msimu mapema mwezi huu akimaliza na pointi moja na kubinjuka mara mbili baada ya dakika 10.
    Pacquiao amesema baada ya mchezo huo kwamba atachukua mapumziko katika timu ya KIA ili kuelekeza nguvu zake katika maandalizi ya pambano lake la kutetea taji lake la WBO uzito wa Welter Novemba 22 mjini Macau dhidi ya bondia ambaye hajapoteza pambano, Chris Algieri bingwa wa uzito wa Welter Junior.
    Na urefu wake wa futi 5 na inchi 6, Pacquiao hana jumbo la kucheza mpira wa kikapu, lakini ni shabiki mkubwa wa mchezo huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANNY PACQUIAO AWEKA NDONDI KANDO NA KUPIGA MPIRA WA KIKAPU, AFANYE MAMBO WE ACHA TU! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top