• HABARI MPYA

    Monday, October 20, 2014

    OKWI, OWINO NA KISIGA WASHINDWA KUFANYA MAZOEZI SIMBA SC LEO, KISA...

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC imefanya mazoezi kwa mara ya kwanza leo tangu sare ya 0-0 na mahasimu wao, Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hata hivyo, wachezaji watatu, beki Joseph Owino, kiungo Shaaban Kisiga na mshambuliaji Emmanuel Okwi hawakufanya mazoezi jioni ya leo viwanja vya Chuo Kikuu, Dar es Salaam.
    Kisiga aliomba udhuru, wakati Okwi aliomba ruhusa ya kumpeleka hospitali Mganda mwenzake, Owino akafanyiwe vipimo.
    Joseph Owino amesababisha Emmanue Okwi asiwepo mazoezini leo

    Kocha Mzambia, Patrick Phiri ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba wachezaji wote hao wana ruhusa yake ya kukosa mazoezi ya leo, lakini kesho watakuwepo.
    “Wameomba ruhusa na shida zao tumezielewa, tumewakubalia, lakini kesho tutakuwa nao mazoezini,”amesema.
    Simba SC baada ya sare nne za mechi zake zote za mwanzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Jumamosi itahamishia mawindo yake mjini Mbeya itakapokuwa mgeni wa Prisons. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OKWI, OWINO NA KISIGA WASHINDWA KUFANYA MAZOEZI SIMBA SC LEO, KISA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top