• HABARI MPYA

    Monday, October 20, 2014

    SARE TASA YA SIMBA NA YANGA, SIMBA YAINGIZA SH MILIONI 427

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    MPAMBANO wa Ligi Kuu ya soka ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya watani wa jadi, Yanga na Simba uliochezwa juzi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umeingiza sh. 427,271,000.
    Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bila kufugana.
    Mashabiki 49,542 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 65,176,932 wakati asilimia 5 ya gharama ya tiketi kwa CRDB ni sh. 21,363,550.

    Kwa upande wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ambayo ni sh. 1,000 kwa kila tiketi, timu mwenyeji Yanga imepata sh. 17,339,700, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 7,431,300 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 24,771,000.
    Mgawo mwingine wa mapato hayo ni Uwanja sh. 43,678,277.67, gharama za mchezo sh. 24,751,024.01, Bodi ya Ligi sh. 23,295,081.42, TFF sh. 17,471,311.07, DRFA sh. 10,191,598.12, timu mwenyeji Yanga sh. 100,460,038.64 na timu ngeni Simba sh. 71,341,186.86.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SARE TASA YA SIMBA NA YANGA, SIMBA YAINGIZA SH MILIONI 427 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top