• HABARI MPYA

    Saturday, November 01, 2014

    KIEMBA, CHANONGO WAMPUUZA RAIS SIMBA SC, KISIGA ATOA UDHURU, WAJUMBE WA KAMATI YA NIDHAMU ‘WACHOMESHWA’ MSIMBAZI

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    WACHEZAJI Amri Kiemba na Haroun Chanongo hawakutokea kwenye kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Simba SC jana bila taarifa yoyote, imeelezwa.
    Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, Kiemba na Chanongo hawakutokea licha ya kutakiwa kufanya hivyo na wala hawajatoa taarifa yoyote.
    “Tuliwaagiza wafike makao makuu ya klabu Saa 4:00 asubuhi (jana), lakini hadi saa 6:00 mchana walikuwa hawajafika na hawakutoa taarifa yoyote, kwa hivyo ikabidi Wajumbe wa Kamati ya Nidhamu watawanyike,”alisema.
    Amri Kiemba hakutokea kikaoni bila taarifa

    Hata hivyo, Aveva alisema baadaye Kisiga alipiga simu kujieleza kwamba amekwama kwenye foleni na waakamuambia hana sababu ya kufika tena, kwa sababu kikao kimeahirishwa.
    Alipoulizwa ni hatua gani watachukuliwa wachezaji hao, Aveva alisema; “Kwanza Kamati ya Nidhamu ilete ripoti ya maandishi kwa Kamati ya Utendaji juu ya kikao chao, baada ya hapo Kamati ya Utendaji itatoa uamuzi,”alisema.
    Watatu hao, Shaaban Kisiga ‘Malone’, Amri Kiemba na Haroun Chanongo waliondolewa kwenye kambi ya Simba SC mapema wiki hii kwa sababu mbalimbali.
    Kisiga alirejeshwa Dar es Salaam kutoka Mbeya kwa tuhuma za kutoa majibu ya kifedhuli kwa uongozi kabla ya mchezo na Prisons Jumamosi, wakati Kiemba na Chanongo wanatuhumiwa kucheza kwa kiwango cha chini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIEMBA, CHANONGO WAMPUUZA RAIS SIMBA SC, KISIGA ATOA UDHURU, WAJUMBE WA KAMATI YA NIDHAMU ‘WACHOMESHWA’ MSIMBAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top