• HABARI MPYA

    Thursday, December 18, 2014

    KIUNGO ZAMBIA ALIYEUMIA AJALINI KUPELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU ZAIDI

    Na Mwandishi Wetu, LUSAKA
    KIUNGO wa Zambia, Changwe Kalale atapelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya kuumia uti wa mgongo ajalini.
    Kalale aliumia uti wa mgongo katika ajali ya gari Desemba 14 akiwa njiani kuelekea kwenye kambi ya taifa ya Zambia mjini Lusaka, ambayo imemfanya apooze.
    Waziri wa Michezo wa Zambia, Chishimba Kambwili amemuambia hayo Kalale na wazazi wake baada ua kumtembelea hospitalini mjini Lusaka jana, kwamba Serikali ya Zambia itahakikisha anapata matibabu mazuri.
    Changwe Kalale akiwa hospitali mjini Lusaka


    “Mchango wako katika mchezo Zambia unatambuliwa na Serikali na tutafanya kila kinachowezekana kukurudisha katika hali yako nzuri. Nilikuwa nina mazungumzo na Kaimu Rais, atakapotulia tutampeleka Afrika Kusini kwa matibabu mazuri,” amesema Kambwili.
    Kiungo huyo mkabaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Zambia anayechezea timu ya Daraja la Kwanza Kaskazini, Chambishi FC ni miongoni mwa wachezaji watatu wa Zambia walioumia baada ya ajali Jumapili.
    Wengine ni beki wa Zesco United, Nyambe Mulenga na kipa Satchmo Chakawa wa Choma Eagles.
    Nyambe amevunjika mguu, wakati Chakawa aliumia mbavu na kibofu cha mkojo.
    Watatu hao walikuwa sehemu ya kikosi cha awali cha wachezaji 24 wa Zambia kilichoteuliwa kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2015 nchini Equatorial Guinea, ambacho kilianza kambi mjini Lusaka Desemba 15.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIUNGO ZAMBIA ALIYEUMIA AJALINI KUPELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top