• HABARI MPYA

    Saturday, December 20, 2014

    SIMBA SC YAIADHIBU ‘KISHIKAJI’ MWADUI YA JULIO, 3-1 ZAWATOSHA WACHIMBA ALMASI

    Na Perincess Asia, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC imeifunga mabao 3-1 Mwadui United ya Shinyanga katika mchezo wa kirafiki, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.
    Katika mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wachache, Simba SC ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza mabao 2-1.
    Ibrahim Hajibu ndiye aliyefunga mabao yote ya Simba SC dakika ya 26 na 37, huku akipoteza nafasi nyingine mbili nzuri za kufunga.
    Bao la Mwadui inayofundishwa na beki na kocha na beki wa zamani wa Simba SC, Jamhuri Kihwelo lilifungwa na Salim Khamis dakika ya 30, baada ya kazi nzuri ya mkongwe Athumani Iddi ‘Chuji’.
    Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza mfungaji wa mabao yao mawili, Ibrahim Hajibu aliyembeba Twaha Ibrahim 'Messi'. Wa pili kulia ni mfungaji wa bao la tatu, Yussuf Baraka. Wengine pichani ni Abdallah Seseme kulia na Said Ndemla kushoto. 

    Kipindi cha pili, Simba SC ilirudi na moto wake na kufanikiwa kupata bao la tatu lililofungwa na kinda wa timu B, Yussuf Baraka dakika ya 76, akimalizia krosi maridadi ya beki Hassan Ramadhan Kessy aliyesajiliwa wiki iliyopita kutoka Mtibwa Sugar.
    Pamoja na kufungwa, Mwadui inayopambana kupanda Ligi Kuu ilicheza vizuri na kuonyesha upinzani dhidi ya Simba SC iliyotumia wachezaji wengi wa akiba, ukiondoa safu ya ulinzi.
    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Hassan Ramadhani Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abulaziz Makame, Joseph Owino/Hassan Isihaka dk46, Said Ndemla, Twaha Ibrahim ‘Messi’, Abdallah Seseme/Awadh Juma dk78, Yussuf Baraka, Ibrahim Hajibu/Shaaban Kisiga ‘Malone’ dk 65 na Iddi Bahati.
    Mwadui United; Mussa Lucheke, Ahmed Mkweche, Adeyum Saleh/Juma Jabu dk71, Amani Kyata/Shaaban Chongo dk46, Joram Mgeveke, Athumani Iddi ‘Chuji’/Amos Emmanuel dk57, Uhuru Suleiman, Razack Khalfan, Kevin Kidukwi, Salim Khamis na Julius Mrope.
    Kiungo wa Mwadui, Uhuru Suleiman akimchezea faulo Ibrahim Hajibu wa Simba SC
    Beki mpya wa Simba SC, Hassan Ramadhani 'Kessy' akiwatoka mabeki wa Mwadui
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAIADHIBU ‘KISHIKAJI’ MWADUI YA JULIO, 3-1 ZAWATOSHA WACHIMBA ALMASI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top