• HABARI MPYA

    Wednesday, January 28, 2015

    KILIMANJARO MARATHON 2015 YAENDELEA KUWA LULU KIMATAIFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MBIO za Kilimanjaro Marathon 2015 zimeendelea kuwa lulu kimataifa ambapo mwaka huu zinatajiwa kuwa na washiriki wa kigeni kutoka nchi zaidi ya 40.
    John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa mbio hizo zinaendelea kuwavutia washiriki wengi wa kimataifa kutokana na jitihada za pamoja zinazofanywa na waandaaji pamoja na bia ya Kilimanjaro Premium Lager katika kutangaza tukio hili. Hii ndio sababu iliyochangia ukuaji wa mbio hizi pamoja na ushiriki kuongezeka kila mwaka.

    Addison alisema washiriki wengi zaidi watatoka Marekani ikifuatiwa na Uingereza. Nchi nyingine zinazotarajiwa kushiriki ni pamoja na Canada, Japan, Uganda, Zimbabwe na Kenya. Nyingine ni pamoja na Sweden, Australia, Hungary, Germany,  Zambia, Morocco, Swaziland, Nigeria na Malawi.
    Zikiwa zimepangwa kufanyika Moshi tarehe 1 Machi 2015, mbio za Kilimanjaro Marathon zitakuwa zimegawanyika katika sehemu nne ambazo ni 42km Kilimanjaro Premium Lager Marathon,  Tigo Kili Half Marathon, Mbio za walemavu za GAPCO Disabled Marathon na 5km Fun Run.
    Mbio hizo pia zinatarajiwa kuchangamshwa na ushiriki wa timu za makampuni ambapo wafanyakazi wa makampuni wadhamini watashindana katika mbio za kilomita 42 na Tigo Kili Half Marathon kupitia shindano litakalojulikana kama“Corporate Challenge”. 
    Addison alisema kuwa mbio za Kilimanjaro Marathon zinaingia katika mwaka wa 13 tangu kuanzishwa zikiwa zimesajiriwa rasmi na shikisho la riadha la kimataifa na kuongeza kuwa kama ilivyo kawaida kutakuwepo na vituo vya maji pamoja na viburudisho vya kutosha katika njia za mashindano hayo.
    “Mbio hii inafanyika chini ya Mlima Kilimanjaro jambo ambalo ni kivutio kikubwa kwa wageni kutoka nchi mbalimbali na inatarajiwa kuwa shamrashamra maana wananchi wengi  watajitokeza kushiriki na wengine pembezoni mwa barabara kuwashangilia na kuwapa moyo washiriki,” Addison aliitimisha.
    Mbio hizo zinaratibiwa na Executive Solutions kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na wadhamini wakuu Kilimanjaro Premium Lager, Tigo (Tigo Kili Half Marathon), GAPCO (Walemavu), Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar,  CMC Automobiles Ltd, RwandAir, FNB Tanzania, Kibo Palace Hotel, UNFPA na Kilimanjaro Water.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KILIMANJARO MARATHON 2015 YAENDELEA KUWA LULU KIMATAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top