• HABARI MPYA

    Tuesday, February 10, 2015

    HANS POPPE ATUPWA NJE TFF, KABURU NA SAID TULIY WAENDELEA KUPETA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MAKAMU wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakati Zacharia Hans Poppe ameenguliwa kwenye Kamati ya Maadili.
    Kwa mujibu wa taarifa ya TFF leo, kikao cha Kamati ya Utendaji Desemba 19, mwaka jana, kilifanya mabadiliko katika kamati ndogo ndogo na zile za kisheria, na kwa bahati nzuri kwake, Mjumbe mwingine wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC, Said Tuliy amebakishwa. 
    Kaburu ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Makamu wake, Ahmed Mgoyi na Wajumbe James Mhagama, Stewart Masima, Steven Njowoka na Sheikh Said Mohammed.
    Lakini Hans Poppe aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Maadili ameenguliwa pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wao, Wakili Richard Sinamtwa, Makamu Wakili Moses Kaluwa na Wajumbe wote Hussein Mwamba, Abdul Sauko, Philemon Ntahilaja na Wakili Imani Madega. 
    Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Maadili ni Wakili Wilson Ogunde, Makamu wake Wakili Juma Nassoro na Wajumbe Wakili Ebenezer Mshana, Geroge Rupia na Mheshimiwa Said Mtanda.
    Zacharia Hans Poppe (kushoto) ameenguliwa Kamati ya Maadili ya TFF

    Kamati nyingine za TFF ni; Kamati Ya Nidhamu Tarimba Abbas (Mwenyekiti) Wakili Jerome Msemwa (Makamu Mwenyekiti) na Wajumbe Kassim Dau, Nassoro Duduma, Kitwana Manara, 
    Kamati Ya Rufani Ya Nidhamu, Wakili Mukirya Nyanduga (Mwenyekiti), Wakili Revocatus Kuuli (Makamu mwenyekiti) na Wajumbe Abdallah Mkumbura,  Dk Franics Michael na Wakili Twaha Mtengela.
    Kamati Ya Rufani Ya Maadili; Wakili Walter Chipeta (Mwenyekiti), Jaji George Kisagenta (Makamu mwenyekiti) na Wajumbe Lilian Kitomari
     Na Wakili Advocate Abdala Gonzi Kamati Ya Uchaguzi, Wakili Melchesedeck Lutema (Mwenyekiti), Adamu Mambi (Makamu mwenyekiti) na Wajumbe Hamidu Mahmoud Omar, Jeremiah John Wambura na John Jembele.
    Kamati Ya Rufani Ta Uchaguzi; Wakili Julius Lugaziya (Mwneyekiti), Wakili Machare Suguta (Makamu Mwenyekiti) na Wajumbe Nassor Idrisa ‘Father’, Paschal Kihanga na Benister Lugora.
    Kamati Ya Fedha Na Mipango; Wallace Karia (Mwenyekiti), Yahya Mohamed (Makamu mwenyekiti) na Wajumbe Goodluck Moshi, Omar Walii, Ellie Mbise na Deo Lubuva, Kamati ya Ufundi, Wilfred Kidao (Mwenyekiti), Athumani Kambi (Makamu mwenyekiti) na Wajumbe  Vedastus Rufano, Oscar Dan Korosso na Pelegriunius Rutahyugwa.
    Kaburu kushoto na Tuliy kulia wamebaki Kamati za TFF

    Kamati Ya Mpira Wa Miguu Ya Vijana; Ayoub Nyenzi (Mwenyekiti), Khalid Abdallah (Makamu mwenyekiti) na Wajumbe Ali Mayay, Mulamu Ngh’ambi na Said Tully, Kamati Ya Mpira Wa Miguu Wanawake; Blassy Kiondo (Mwenyekiti), Rose Kissiwa (Makamu mwenyekiti) na Wajumbe Zena Chande, Amina Karuma, Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma na Ingrid Kimario (Katibu wa Kamati).
    Kamati Ya Waamuzi; Saloum Umande Chama (Mwenyekiti), Nassoro Said (Makamu mwenyekiti) na Wajumbe Charles Ndagala (Katibu), Kanali Issaro Chacha na Soud Abdi, Kamati Ya Habari Na Masoko, Athuman Kambi (Mwenyekiti), Almasi Kasongo (Makamu Mwenyekiti), Rose Mwakitangwe, Amir Mhando na Haroub Selemani.
    Kamati Ya Ukaguzi Wa Fedha;  Ramdhan Nassib (Mwenyekiti), Epaphra Swai (Makamu mwenyekiti) na Wajumbe Jackson Songora, Golden Sanga, Francis Ndulane na Cyprian Kwiyava.
    Kamati Ya Tiba; Dk Paul Marealle (Mwenyekiti) Dk Fred Limbanga (Makamu mwenyekiti), na Wajumbe Dk Mwanandi Mwankewa,  Dk Eliezer Ndelema na Asha Mecky Sadik, Kamati Ya Futsal Na Beach Soccer;  Ahmed Idd Mgoyi (Mwenyekiti), Hussein Mwamba (Makamu mwenyekiti) na Wajumbe Samson Kaliro, Shaffih Dauda, Boniface Pawassa na Apollo Kayugi.
    Kamati ya Shughuli Maalum, Omar Abdulkadir (Mwenyekiti), Emmanuel Chaula (Makamu mwenyekiti) na Wajumbe Victor Mwandike, Riziki Majala, Zahra Mohamed na David Nyandu, Kamati ya Uwekezaji na Biashara, William Erio (Mwenyekiti), Mbaraka Igangula, Wakili Imani Madega, Luteni Kanali Charles Mbuge na Philemon Ntalihaja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HANS POPPE ATUPWA NJE TFF, KABURU NA SAID TULIY WAENDELEA KUPETA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top