• HABARI MPYA

    Monday, March 02, 2015

    AZAM TV WAMWAGA NEEMA LIGI DARAJA LA KWANZA

    Na Asha Said, DAR ES SALAAM
    KAMPUNI ya Azam Media Group Limited, kupitia Televisheni ya Azam TV imefikia makubaliano na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) kuwa wadhamini wakuu wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara. 
    Hata hivyo, vipengele vya Mkataba kwa maana ya dau la udhamini, masharti na namna ambavyo klabu na mdhamini watanufaika, vitatajwa baadaye.   
    Kaimu Mtendaji wa Bodi hiyo, Fatma Shibo alisema hilo liliwekwa wazi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TPLB pamoja na klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza, uliofanyika Februali 28, mwaka huu.
    Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group, Rhys Torrington (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Yussuf Bakhresa (kulia)


    Fatma Shibo, alisema kuwa katika mkutano huo, kulijadiliwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na utendaji wa bodi hiyo.
    Alisema kuwa mambo mengine yaliyojadiliwa ni vurugu za zinazotokea viwanjani, maoni ya klabu kuhusu viwanja vinavyotumika kwa ligi hizo.
    Shibo alisema kuwa klabu za ligi kuu zililalamikia 
    mfomu wa tiketi za Kieletroniki, ambapo klabu 
    zimelalamikia mapato kupungua kwa asilimia 40.
    Alisema Bodi ya ligi imelichukua hilo na kulifanyia kazi kwa kuwa ilikuwa tayari imeanza mazungumzo na benki inayohusika na utengezwaji wa tiketi ya CRDB, mapmoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    Shibo alisema kuwa katika mkutano huo, klabu za Ligi Daraja la Kwanza nazo zimepata mdhamini ambaye ni kampuni ya TV ya Azam Tv, ambayo, msimu ujao itakuwa inaonyesha mechi za ligi hiyo. 
    Katika suala la malalamiko ya waamuzi, tayari kamati ya utendaji ya TFF, iliteuwa kamati maalum, ambayo itakuwa ikifuatilia na kutoa maamuzi ndani ya masaa 75. 
    Alisema kamati hiyo imemteua Sheikh Said Mohamed, ambaye ni Mwenyekiti wakati makamu wake ni Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na wajumbe ni Charles Ndagala na Steven Mguto. 
    "Katika mkutano huo suala la waamuzi na tiketi 
    zilichukua nafasi kubwa kwa sababu klabu zinadai 
    mapato kupungua kwa asilia 40, hivyo bodi ya ligi, TFF na CRDB, tunaendelea kufanya vikao, vya kutatua tatizo hilo"alisema Shibo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM TV WAMWAGA NEEMA LIGI DARAJA LA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top