• HABARI MPYA

    Wednesday, March 25, 2015

    MESSI NDIYE MWANASOKA 'MKUNJA MKWANJA MNENE' DUNIA NZIMA, MOURNHO ATISHA KWA MAKOCHA

    MSHAMBULIAJI wa Bracelona, Lionel Messi ndiye mchezaji anayelipwa zaidi kwa sasa duniani, akiwa anaingiza karibu Pauni Milioni 1 kwa wiki kutokana na mshahara na mikataba ya udhamini.
    Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina aliingiza pauni Milioni 47.8 mwaka 2014 za udhamini pamoja na mshahara wa klabu yake, Pauni Milioni 26.
    Miongoni mwa wadhamini wa Messi ni Adidas, FIFA 15 na Turkish Airlines na hiyo inampandisha juu ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Ureno. Mreno huyo, Ronaldo, aliingiza Pauni Milioni 39.7, kwa mujibu wa taarifa zilizotoka sasa za Jarida la Wanasoka Tajiri.
    Kwa upande wa makocha, Mreno Jose Mourinho wa Chelsea ndiye anaongoza pato lake la mwaka likiwa ni Pauni Milioni 13.2, akifuatiwa na Mtaliano wa Real Madrid, Carlo Ancelotti Pauni Milioni 11.4, Mspanyola wa Bayern Munich, Pep Guardiola Pauni Milioni 11.2, Mfaransa wa Arsenal, Arsene Wenger Pauni Milioni 8.3 na Mholanzi wa Manchester United, Louis van Gaal Pauni Milioni 7.3.
    Messi tops up his salary with Barcelona by promoting various companies, including adidas 
    Lionel Messi anaongoza kwa utajiri miongoni mwa wanasoka duniani  
    Cristiano Ronaldo comes in second in the annual France Football list with earnings of £39.7m
    Cristiano Ronaldo anashika nafasi ya pili kwa Pauni zake Milioni 39.7

    WACHEZAJI WANAOLIPWA ZAIDI DUNIANI 

    1. Lionel Messi Pauni Milioni 47.8
    2. Cristiano Ronaldo Pauni Milioni 39.7
    3. Neymar Pauni Milioni 26.8
    4. Thiago Silva Pauni Milioni 20.2
    5. Robin van Persie Pauni  Milioni 18.8
    6. Gareth Bale Pauni Milioni 17.5
    7. Wayne Rooney Pauni Milioni 16.5
    8. Zlatan Ibrahimovic Pauni Milioni 15.8
    9. Sergio Aguero Pauni Milioni 15.6
    10. Robert Lewandowski Pauni Milioni 14.8 kwa mwaka 

    MAKOCHA WANAOLIPWA ZAIDI DUNIANI 

    1. Jose Mourinho Pauni  Milioni 13.2 kwa mwaka
    2. Carlo Ancelotti Pauni Milioni 11.4
    3. Pep Guardiola Pauni Milioni 11.2
    4. Arsene Wenger Pauni Milioni 8.3
    5. Louis van Gaal Pauni Milioni 7.3
    6. Fabio Capello Pauni Milioni 6.6
    7. Andre Villas-Boas Pauni Milioni 6.2
    8. Sven-Goran Eriksson Pauni Milioni 5.9
    9. Jurgen Klopp Pauni Milioni 5.3
    10. David Moyes na Laurent Blanc Pauni Milioni 5.1 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MESSI NDIYE MWANASOKA 'MKUNJA MKWANJA MNENE' DUNIA NZIMA, MOURNHO ATISHA KWA MAKOCHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top