• HABARI MPYA

    Wednesday, March 25, 2015

    PAMBANO LA CANNAVARO NA JUMA ABDUL LEO TAIFA…

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BEKI wa kulia wa Yanga SC, Juma Abdul leo ameonyesha utovu wa nidhamu baada ya kupigana na Nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Tukio hilo lilitokea wakati wa mapumziko, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya timu hiyo na JKT Ruvu.
    Na ilitokana na timu hiyo kufungwa bao dakika ya 45 na Samuel Kamuntu wa JKT, kutokana na makosa ya Juma Abdul na kufanya dakika 45 za kipindi cha kwanza, zimalizike Yanga ikiwa mbele kwa mabao 2-1. 
    Cannavaro alikwenda kumlaumu Juma Abdul kutokana na kosa alilolifanya hadi JKT wakapata bao, lakini Nahodha huyo wa Wana Jangwani alijuta kwa kitendo hicho, kwani ‘aliporomoshewa mvua ya matusi’ na mchezaji mwenzake huyo.
    Niacheni nimpe kichapo Mpemba huyu; Ilibidi nguvu zitumike kumdhibiti Juma Abdul asiendelee kupigana na Nahodha wake
    Usiniletee na wewe, Ntakuzingua; Juma Abdul (kushoto) akimpandishia Simon Msuva (katikati) ambaye alikuwa anamsihi aache kuzozana na Nahodha wake. Kulia ni Mrisho Ngassa ambaye sura yake inaeleza kila kitu
    Chunga sana dogo, ntakuumiza; Nahodha Cannavaro akijibizana na Juma Abdul, huku wachezaji wenzake wakimsihi aache
    Acha hasira Juma; Meneja Hafidh Saleh akimpeleka chumbani Juma Abdul kuepusha shari zaidi


    Cannavaro hakuweza kuvumilia, akajikuta anajibizana matusi na Juma Abdul wakati wanatoka uwanjani kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
    Na walipofika kwenye sebule ya kuelekea kwenye chumba chao cha kubadilishia nguo, ndipo wakavaana na kuanza kutupiana makonde.
    Hata hivyo, wachezaji wenzao na viongozi wa benchi la Ufundi la klabu hiyo wakiongozwa na Meneja, Hafidh Saleh waliwaachanisha.
    Baada ya kufika kwenye chumba chao, makocha wa timu hiyo, Mholanzi Hans van der Pluijm na Mzalendo, Charles Boniface Mkwasa waliwapa maneno ya hekima ya kuwasuluhisha ili warudishe akili zao mchezoni. Wote walirejea uwanjani na kumalizia sehemu iliyobaki ya mchezo, Yanga SC ikishinda 3-1.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAMBANO LA CANNAVARO NA JUMA ABDUL LEO TAIFA… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top