• HABARI MPYA

    Wednesday, March 04, 2015

    TFF WAIZODOA YANGA ‘ISHU’ YA HAJIB, YAWAAMBIA NA WAO WAKITAKA WAOMBE TU

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeitaka Yanga SC kutojisumbua kuhusu Simba SC kumchezesha mshambuliaji wake Ibrahim Hajib Migomba akiwa ana kadi tatu za njano, kwani taratibu zilifuatwa.
    Akilitolea ufafanuzi hilo, Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa amesema mchakato wa kumpatia ruhusa Hajib hauna mashaka ambapo endapo Yanga wanataka kitu kama hicho wanatakiwa wawahi mapema.
    "Hakuna mashaka katika hilo, kila kitu kipo sawa hiyo kanuni ilipitishwa na imeanza kutumika hata wao Yanga kama wanataka wanatakiwa kuwahi kutuletea mapema siku moja kabla ya mchezo,"alisema Mwesigwa.
    Ibrahim Hajib kulia analalamikiwa na Yanga SC kucheza akiwa ana kadi tatu za njano


    Yanga SC inalalamika juu ya Bodi ya ligi kuruhsu Hajib acheze akiwa ana kadi tatu za njano, lakini hawajui kwamba Wekundu hao walianza mapema kutumia kanuni hiyo kwa kumchezesha kiraka Abdi Banda akiwa ana kadi tatu pia za njano.
    Yanga leo kupitia Mkuu wa Kitengo chake cha Habari na Mawasiliano, Jerry Muro imepinga uamuzi wa kumchezesha Hajib katika mchezo dhidi ya Prisons akiwa na kadi tatu za njano.
    Yanga SC imesema Hajib amefikisha kadi nne sasa baada ya kuonyeshwa kadi nyingine katika mchezo dhidi ya Prisons Jumamosi iliyopita, akifunga mabao matatu katika ushindi wa 5-0.
    Wakati Yanga ikilalamika hivyo BIN ZUBEIRY imepata taarifa kwamba Simba ilianza mapema kutumia kanuni hiyo wakati ikicheza dhidi ya Stand United Februari 22, mwaka huu kwa kumuombea kibali kama hicho Banda aliyekuwa akiwa ana kadi tatu za njano kabla ya mchezo huo.
    Katika kibali hicho ambacho Simba walipewa na Bodi ya Ligi, Banda alitakiwa asichezeshwe katika mchezo dhidi ya Prisons ambao mchezaji huyo alikaa jukwaani
    "Yanga wanashangaza mbona wanashituka muda umepita, tulianza kutumia fursa hiyo mapema kwa kumchezesha Banda ambaye tuliombea kibali kama hicho cha Hajib,"alisema kiongozi mmoja wa Simba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF WAIZODOA YANGA ‘ISHU’ YA HAJIB, YAWAAMBIA NA WAO WAKITAKA WAOMBE TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top