• HABARI MPYA

    Monday, March 02, 2015

    MALINZI 'AWAPA GWALA' MALI KUBEBA MWALI WA MAKINDA AFRIKA

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shrikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Rais Boubacar Diara wa Shirikisho la Soka Mali (FMF) kwa kutwaa Ubingwa wa Afrika kwa vijana U17.
    Katika salam zake, Malinzi amesema mafanikio mazuri waliyoyapata FMF yametokana na uongozi bora, kamati ya utendaji na mipango thabiti waliyoiweka katika soka la Vijana.
    Kwa kutwaa Ubingwa wa vijana Afrika U17, Mali wamepata nafasi ya kuliwakilisha Bara la Afrika kwenye fainali za U17 za Dunia nchini Chile pamoja na nchi za Afrika Kusini, Guinea na Nigeria.
    Mali wametwaa Ubingwa wa vijana Afrika U17 baada ya kuifunga timu ya taifa ya vijana ya Afrika Kusini (Amajimbo's) kwa mabao 2-0.
    “Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu, TFF na Watanzania wote, tunawapa pongezi FMF kwa kutwaa Ubingwa huo,”amesema Malinzi, ambaye pia amempongeza Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA), Dany Jordaan kwa timu ya Amajimbo's kushika nafasi ya pili.
    Amajimbo's ndio timu pekee kusini mwa Bara la Afrika watakaowaklisha kwenye fainali za U17 za Dunia nchini Chile Oktoba mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI 'AWAPA GWALA' MALI KUBEBA MWALI WA MAKINDA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top