• HABARI MPYA

    Tuesday, April 14, 2015

    KOPUNOVIC AMKATAA MAZOEZINI KESSY, AMUONDOA KWENYE PROGRAMU YA MBEYA CITY

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Simba SC, Mserbia Goran Kopunovic leo amekataa kumpokea mazoezini beki Hassan Ramadhani Kessy baada ya kuchelewa na amesema amemuondoa kwenye programu ya mchezo ujao dhidi ya Mbeya City.
    Simba SC inajiandaa na mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
    Na kikosi cha Kopunovic kilikuwa kinaendelea na mazoezi Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na wachezaji wote waliwahi kufika kwa mujibu wa ratiba, kasoro Kessy.
    Hassan Kessy ameondolewa kwenye programu ya mechi ya Mbeya City
    Kocha Mserbia, Goran Kopunovic (kushoto) akiwa na Msaidizi wake, Suleiman Matola kulia 

    Kessy alifika wakati wenzake wamekwishaanza mazoezi na alipotaka kuungana nao, kocha Mserbia akamzuia. Kopunovic akamuagiza kocha Msaidizi, Suleiman Matola azungumze na mchezaji huyo kujua kilichomfanya achelewe.
    Baada ya Matola kumaliza mazungumzo na beki huyo wa pembeni, alikwenda kumpa ujumbe Kopunovic, ambaye alionekana kutoridhishwa na utetezi uliotolewa. 
    Kaponovic akamuamuru Kessy afanye mazoezi ya peke yake kuuzunguka Uwanja na baada ya mechi akasema; “Kwa ujumla sijafurahishwa na nihdamu ya huyu mchezaji, na nimemuondoa kwenye programu ya mechi ya Mbeya City, hatakwenda”.
    Kessy anakumbana na ‘kasheshe’ hilo wakati ndiyo kwanza, alikua anaungana na wenzake leo baada ya kususa kwa zaidi ya wiki mbili, akishinikiza apewe salio la fedha zake za usajili Sh. Milioni 5, baada ya awali kupewa Milioni 15 baada ya kusaini Mkataba wa miaka miwili Desemba mwaka jana pamoja na nyumba ya kuishi.  
    Pamoja na sakata lake kutaka kugeuka mgogoro baina yake na klabu hiyo, lakini mazungumzo baina ya pande hizo mbili yalileta suluhu na mchezaji huyo akakubali kurudi kazini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOPUNOVIC AMKATAA MAZOEZINI KESSY, AMUONDOA KWENYE PROGRAMU YA MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top